Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc, Sabasaba Moshingi (katikati)
akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered,
Sanjay Rughani wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya miezi tisa ya program ya
Mwanamke wa Wakati Ujao ya kundi la pili yanayoendeshwa na Chama cha
Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya
Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo yana
lengo la kuwaandaa wafanyakazi wanawake kushika nafasi za juu za uongozi
katika makampuni na bodi za wakurugenzi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ATE, Bi. Jayne Nyimbo (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara ya
Sheria ya ATE, Suzan Ndomba (kushoto) ma Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk.
Aggrey Mlimuka (katikati), wakifurahi na Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na
maendeleo wa Acacia Mining, Janeth Lekashingo katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bi. Jayne Nyimbo (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzu wa Kampuni ya Statoil Tz, Gunnar Mentzsen huku
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani
akiangalia wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya program ya Mwanamke wa
Wakati Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa
kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO)
jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Taasisi ya Uongozi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI), Prof. Apollonia
Kerenge (kulia), akizungumza na washiriki wa kundi la pili wa mafunzo
ya miezi tisa ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao yanayoendeshwa na
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shireikisho la
Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo
yana lengo la kuwaandaa wafanyakazi wanawake kushika nafasi za juu za
uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Mugeta (kulia), akizungumza
na washiriki wa mafunzo ya miezi tisa ya program ya Mwanamke wa Wakati
Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa
kushirikiana na Shireikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO)
jijini Dar es Salaam juzi. Mafunzo yana lengo la kuwaandaa wafanyakazi
wanawake kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za
wakurugenzi.
Mratibu
wa Program ya Mwanamke wa Wakati Ujao ya Chama cha Waajiri Tanzania
(ATE), Bi. Lilian Machera akizungumza na washiriki hao kuhusu utaratibu
wa mafunzo hayo yenye malengo ya kuwaandaa wafanyakazi wanawake kushika
nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.
Mmoja
wa washiriki wa mafunzo ya program ya Wanawake wa Wakati Ujao, Bi. Anna
Nyimbo akijitambulisha kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo yatakayochukua
kipindi cha miezi tisa.
Washiriki
wa kundi la pili la mafunzo ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao
wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya viongozi wa ATE pamoja
na wakurugenzi wa makampuni 16 yanayofadhili mafunzo hayo. Makampuni
hayo ni; Acacia Mining,
Alistair Equipment Services (T) Ltd, AngloGold Ashanti, Geita Gold Mine,
Cartrack Tanzania Limited, EFC Microfinance Bank, Ubalozi wa Denmark,
Global Health Program-Tanzania, HJFMRI, Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Benki ya NMB Plc, Mfuko wa PPF , Songas Limited, Benki ya
Standard Chartered, Statoil Tanzania AS, Benki ya TIB Corporate, Benki
ya TPB Bank Plc na Under The Same Sun.
No comments:
Post a Comment