RAIS
Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha
kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo asimamishwe kazi kwa
tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya
kuishi kinyume cha taratibu.
Kauli
hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Julai 28, 2017), na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao
hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu
Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea wakati wa kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea wakati wa kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala na Makamishna wa Idara hiyo baada ya kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Amesema
haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya
kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. “Idara ya Uhamiaji
tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila
ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu
Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.”
Waziri
Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini jambo hilo kwa
kina: “Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao
ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa
mapenzi yake tu...Sasa hii ni dosari hatuwezi kuivumilia.”
Amesema
Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji
raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na
uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.
"Hawa
Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini
wameingia tu na kupewa vibali. Hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli
ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani
kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."
Pia
Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo cha utoaji
hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. "
Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri
ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika
ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya."
Hata
hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa watu wote
walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi kama wanakidhi
matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwasili Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam.Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea wakati wa kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea wakati wa kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiendela kutoa maagizo kwa Waziri wa Mambo
ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala na Makamishna wa Idara hiyo baada ya kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala na Makamishna wa Idara hiyo baada ya kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala.
Picha na habari na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment