Halmashauri
ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imezindua visima vitano virefu
vyenye thamani ya zaidi ya milioni hamsini vilivyotolewa msaada na
ubalozi wa Kuwait nchini.
Visima hivyo vitano vilivyozinduliwa vimejengwa katika kijiji cha Kisayani, Kerekese, Mpafu, Sotele na Sangasanga vya Mkuranga.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo wilayani mkuranga mkoani pwani balozi wa Kuwait
Mhe. Jasem Al-Najem alisema serikali ya Kuwait kupitia ubalozi uliyopo
nchini inafanya jitihada kubwa kusaidia Tanzania katika nyanja
mbalimbali zinazohusu Jamii ikiwemo afya pamoja na maji.
Aidha
balozi Jasem alisema katika kuunga mkono sera ya Rais wa awamu ya tano
Dkt John Pombe Magufuli ya elimu bure wameamua kuanzisha mradi
ujulilanao wa kisima kila shule ili kupinguza changamoto ya maji pamoja
na kuakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama kwa wakati lengo
nikuboresha elimu nchini."maji no muhimu sana uchimbaji wa maji
mashuleni sio utasaidia wanafunzi na wanachi wanaoishi karibu na
kusaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kupata huduma kamili ya
masomo"alisema.
Pia
ubalozi huo umetoa mabeseni hamsini pamoja na vifaa vya akina mama
wakati wa kujifungua katika hospital ya wilaya ya mkuranga ili kuboresha
huduma ya afya.
Aidha
Mbunge wa viti maalum mkoa wa pwani Zainabu Vulu alisema afya ya Mama
na mtoto ni muhimu sana na kukikosekana vifaa afya ya mama itakuwa
hatarishi."tunashukuru sana kwa msaada wenu huu utasaidia sana mama
kujifungua mtoto mwenye afya na mwenyewe kubaki mwenye afya "alisema.
Hata
hivyo Mbunge wa jimbo la mkuranga mh. Abdalah Hamis Ulega amewashuru
kuwait kwa msaada huo na kusema mpaka sasa wameshachimba visima ishirini
visima nane kati ya hivyo ni vya serikali.
Aidha
aliongeza kama Mbunge wa mkuranga aliguswa na kuamua kutafuta wafadhili
baada ya kupata barua kutoka kwa Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
kisayani kutaka kuifunga shule hiyo kutokana na changamoto ya maji,ndipo
akawatafuta wafadhili hao ambao wamechima visima virefu vitano vya maji
wilayani humo.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya mkuranga Filiberto Sanga alitoa wito kwa
wanachi kuhakikisha wanakitunza kisima hicho kisiharibike.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Sanga akizunguma na wanacnhi wa
kijiji cha Mpafu katika hafala ya uzidunzi wa visima vitano vyenye
thamani ya zaidi ya milioni hamsini vilivyotolewa msaada na ubalozi wa
Kuwait nchini Visima hivyo vitano vilivyozinduliwa vimejengwa katika
vijiji vya Kisayani, Kerekese, Mpafu, Sotele na Sangasanga
Balozi
wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akizungumza na wanchi wa kijiji
cha Mpafu kataika uzinduzi wa visima virefu vitano vilivyo fadhiliwa na
Ubalozo wa Kuwet nchini leo mkoani Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega akimshukuru Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jaseem Al Najem kwakuchimba visima hivyo.
Mganga
Mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo wa (kwanza kushoto)
akitoa maelekezo mbele ya Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al
Najem,watendaji wakuu wa wilaya katika hafla ya uzidunzi wa visima
virefu vitano vilivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni hamsini.
Balozi
wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem wa (pili kushoto) akikabidhi
watendaji wa wilaya ya mkuranga mabeseni hamsini pamoja na vifaa vya
akina mama wakati wa kujifungua katika hospital ya wilaya hiyo.Picha
zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Balozi
wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akizindua kisima katika kijiji
cha Mpafu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga,
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega.
Picha ya pamoja
Balozi
wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem wakionja maji baada ya kuzindua
kisima katika kijiji cha Mpafu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya
Mkuranga,Filberto Sanga, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah ulega.
Picha na habari na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii
No comments:
Post a Comment