Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Imepongezwa na kushukuriwa
na watu wenye ulemavu wa kutoona, kwa kuwakomboa kutoka walemavu omba
omba, na kuwageuza kuwa ni wajasiliamali wanaojitegemea na kuchangia
maendeleo ya Taifa.
Pongezi
hizo, zimetolewa na wahitimu wa kwanza, wa mafunzo ya kushona nguo kwa
wasiona, yaliyofadhiliwa na TANTRADE na kuendeshwa na mtu asiyeona,
Abdala Nyangarika, wakati wa mahafali yaliyofanyika jana katika viwanja
vya Tantrade, Kilwa Rd, jijini Dar es Salaam.
Wahitimu
hao, wamezitoa pongezi hizo katika risala yao, iliyosomwa na mmoja wao,
Philemon Isaka, ambao kwanza waliishukuru na kuipongeza TANTRADE kwa
kuwathamini watu wenye ulemavu, kisha kujitolea kuwakomboa kwa
kuwajengea uwezo, wa kujitegemea, hivyo kuwaepusha kugeuka omba omba.
Ila pia wametoa wito kwa jamii, kuungana na TANTRADE kuwapatia vifaa ili
waweze kujitegemea. TANTRADE imejitolea kuwapatia mafunzo tuu, lakini
ili waweze kujitegemea, jamii imeombwa kuwapatia vyerehani na mitaji,
ili ujuzi walioupata, uweze kuwasaidia kujitegemea na kuchangia
maendeleo.
Wahitimu
wa mafunzo ya kushona nguo kwa wasiiona, wakiwa kwenye picha ya pamoja
wakiwa na na nyuso za furaha, wakionyesha vyeti vyao vya kuhitimu
mafunzo ya kushona kwa cherehani kwa watu wenye ulemavu wa kutoona,
baada ya kuhitimu mafunzo haya ya miezi 6, , yaliyoendeshwa na mkufunzi
mwenye ulemavu, Dr. Abdalah Nyangalio na kufadhiliwa na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE. Wahitimu hao, wameomba jamii
iwasaidie kupata cherehani ili waweze kuutumia ujuzi walioupata,
kujitegemea badala ya kuendelea kuwa omba omba.
Kwa
Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Edwin Rutageruka, baada ya
TANTRADE kugundua kipaji cha kushona cha Abdala Nyangalio, mwenye
ulemavu wa kutoona, ilimpatia fursa kushiriki maonyesho ya sabasaba, na
maonyesho mbalimbali ya nje ya nchi, ndipo ikaamua kuanzisha mafunzo
hayo ili kuutumia utaalamu wa Nyangalilo kuwasaidia wasiona wengine
wenye vipaji vya ushonaji bila kujijua.
Rutageruka
ametoa wito kwa Jamii kujitokeza kununua bidhaa za walemavu hawa, ili
kuwaunga mkono, na kwa upande wake, amesema TANTRADE itaendelea
kuwafungulia fursa, watu wenye ulemavu, ili kuvitumia vipaji vyao
mbalimbali kuzalisha mali, kwa kuwaunganisha na masoko kupitia
maonyesho ya Saba Sana, na kuwapeleka soko la Afrika ya Mashariki
hatimaye kuzitumia fursa za soko la AGOA.
Mgeni
rasmi ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, aliyewakilishwa na Kaimu Katibu
Tawala wa Wilaya ya Temeke, Mafuku Kabeya, ameipongeza TANTRADE kwa
kuanzisha mafunzo hayo, na kutoa wito kwa jamii na taasisi ziunge mkono
juhudi za TANTRADE ili kutanua wigo wa mafunzo hayo kuwafikia
walemavu wengine mbalimbali wenye vipaji, kuwafundisha wengine
kujitegemea na kuchangia maendeleo ya taifa.
Mkufunzi
wa mafunzo ya kushona kwa wasiiona, ambaye yeye mwenyewe haoni, Dr.
Abdalah Nyangalio akimuonyesha Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala wa
Wilaya ya Temeke Mafuku Kabeya, (katikati), nguo zilizoshonwa na watu
wenye ulemavu wa kutoona, walizoshona kwa cherehani, baada ya kuhitimu
mafunzo haya ya miezi 6, yaliyo fadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania, Tantrade. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE,
Edwin Rutageruka. Wahitimu hao, wameomba jamii iwasaidie kupata
cherehani ili waweze kuutumia ujuzi walioupata, kujitegemea badala ya
kuendelea kuwa omba omba.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wasiona cha Mkoa wa Dar es Salaam,Alex Lwimbo, ameiomba
jamii na taasisi kujitolea kusaidia uwezeshaji ya watu wenye ulemavu,
ili waweze kujitegemea, kwa hoja kuwa walemavu wakiwezeshwa, wanaweza.
Na
mwisho ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Abdala Nyangalio, ambaye amepewa
jina la utani ya Dr. Nyangalio, ambaye ni fundi cherehani asiyeona,
akasema kila mwenye ulemavu Fulani, pia ana kipaji Fulani kufidia
ulemavu huo, hivyi jukumu la jamii kwanza kubaini vipaji hivyo, kisha
kuwajengea uwezo kwa kuwawezesha kutumia kipaji hicho. Hivyo yeye
anatumia kipaji chake, kuwafundisha walemavu wengine wasioona, lakini
wana vipaji.
Bwana
Nyangalio, akamalizia kwa kutoa ombi maalum kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli, kuunga mkono juhudi zao,
kwa kuwatembelea kwenye mafunzo hayo ili wampime suti maalum,
atakapoivaa, itahamasisha watu kununua nguo za wenye ulemavu
Mafunzo
hayo yanaendeshwa kwa awamu mbalimbali, na kazi za ushonaji za walemavu
hao, zitaonyeshwa kwenye Banda la Tanzania, kwenye Maonyesho ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoanza wiki tatu zijazo,
hivyo Jamii imehamasishwa, kuja kushuhudia maajabu haya.
Wahitimu
wa mafunzo ya kushona nguo kwa wasiiona, wakiwa na nyuso za furaha,
wakionyesha nguo walizoshona kwa cherehani, baada ya kuhitimu mafunzo
haya ya miezi 6, , yaliyoendeshwa na mkufunzi mwenye ulemavu, Dr.
Abdalah Nyangalio na fadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania, TANTRADE. Wahitimu hao, wameomba jamii iwasaidie kupata
cherehani ili waweze kuutumia ujuzi walioupata, kujitegemea badala ya
kuendelea kuwa omba omba.
Mgeni
rasmi kwenye kozi ya ushonaji kwa wasiiona, Kaimu Katibu Tawala wa
Wilaya ya Temeke Mafuku Kabeya, (katikati), akitunuku cheti cha kuhitimu
mafunzo ya kushona nguo kwa cherehani kwa watu wenye ulemavu wa
kutoona, kwa mhitimu, Neema Mahonya, baada ya kuhitimu mafunzo ya miezi
6, yaliyoendeshwa na mkufunzi mwenye ulemavu, Dr. Abdalah Nyangalio.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania,
Tantrade. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona cha Mkoa
wa Dar es Salaam, Alex Lwimbo, Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Dr. Abdalah
Nyangalio,(wa pili Kulia), na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE,
Edwin Rutageruka.
Mgeni
rasmi kwenye kozi ya ushonaji kwa wasiiona, Kaimu Katibu Tawala wa
Wilaya ya Temeke Mafuku Kabeya, (katikati), akishuhudia jinsi watu wenye
ulemavu wa kutoona, wanavyoshona nguo kwa cherehani, baada ya kuhitimu
mafunzo ya miezi 6, yaliyoendeshwa na mkufunzi mwenye ulemavu, Dr.
Abdalah Nyangalio. Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania, Tantrade. Wa kwanza kulia ni Mkufunzi wa Mafunzo
hayo, Dr. Abdalah Nyangalio, na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE,
Edwin Rutageruka.
Mgeni
rasmi kwenye kozi ya ushonaji kwa wasiiona, Kaimu Katibu Tawala wa
Wilaya ya Temeke Mafuku Kabeya, (katikati), akitunuku cheti cha kuhitimu
mafunzo ya kushona nguo kwa cherehani kwa watu wenye ulemavu wa
kutoona, kwa mhitimu, Philemon Isaka, baada ya kuhitimu mafunzo ya miezi
6, yaliyoendeshwa na mkufunzi mwenye ulemavu, Dr. Abdalah Nyangalio.
Isaka amesindikizwa na Mkufunzi msaidizi wa kozi hiyo, Helelinda
Nyandindi, ambaye ndiye pekee mwenye kuona kuwasaidia wasiiona kushona.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania, Tantrade. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona
cha Mkoa wa Dar es Salaam, Alex Lwimbo, Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Dr.
Abdalah Nyangalio,(wa pili Kulia), na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa
TANTRADE, Edwin Rutageruka.
No comments:
Post a Comment