Na Stella Kalinga, Simiyu
Shirika
la Kidini la Madhebu ya Kikristo la Life Ministry limetoa vifaa tiba
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 40 kwa Hospitali Teule ya
Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Akipokea
vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Life
Ministry kwa msaada huo na kuwahakikishia kuwa vifaa hivyo vitasaidia
kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi katika hospitali hiyo.
Aidha,
amesema Serikali iko tayari kushirikiana na madhehebu ya dini katika
kuhakikisha kuwa afya za wananchi zinakuwa salama, hivyo
akawahakikishia kuwa milango iko wazi kwa taasisi nyingine za dini
zinazotaka kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za
afya.
Mtaka
ameongeza kuwa ili Madaktari na wauguzi waweze kutekeleza majukumu yao
vizuri ni lazima wawezeshwe vifaa, hivyo msaada huo utawatia moyo na
kuongeza ari ya kufanya kazi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Life Ministry hapa nchini, Dismas Shekalaghe
amesema vifaa hivyo vimetolewa kama sehemu ya kuisaidia jamii ambavyo
vitawawezesha madaktari na wauguzi kuwahudumia wananchi.
Shekalaghe
ameongeza kuwa wao wanaamini kuwa ili mtu aweze kumtumikia Mungu ni
lazima awe na afya njema, hivyo kupitia msaada huo wa vifaa wagonjwa
watahudumiwa na kurudi katika hali zao kawaida na kuendelea kumtumikia
Mungu na kufanya shughuli za maendeleo.
Naye
Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, Dkt.Fredrick
Mlekwa akitoa shukrani kwa Life Ministry amesema, msaada huo umefika
katika wakati muafaka ambapo amesisitiza kuwa uongozi wa Hospitali
umefarijika kupata vifaa hivyo ambavyo vitawasaidia kutoa huduma bora
kwa wananchi.
“Tumefarijika
sana kupata msaada huu na walengwa ambao ni wananchi watapata huduma
bora kupitia vifaa hivi, naomba nitoe wito kwa Mashirika mengine ya
madhehebu ya dini kuendelea kutusaidia kwa kuwa Hospitali hii
inawahudumia watu wenye mahitaji mbalimbali” alisema Dkt.Mlekwa.
Baadhi
ya Vifaa vilivyotolewa na Life Minisry ni pamoja na viti vya kubebea
wagonjwa(wheel chairs), vifaa vya viungo bandia, vifaa vya huduma za
meno, vifaa vya vinavyotumika katika upasuaji, bandeji na mabomba ya
sindano.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa
Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakipokea baadhi
ya vifaa vilivyotolewa Life Ministry kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika
hilo la dini, Bw. Dismas Shekalaghe(Kulia).
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa
Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakikabidhiwa
viti vya kubebea wagonjwa na Mkurugenzi wa Life Ministry Bw. Dismas
Shekalaghe (kulia). ambavyo ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa
Shirika hilo la Kikristo kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wachungaji wa
madhehebu ya Kikristo wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa
na Shirika la Kikristo la Life Ministry kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa
Simiyu, mjini Bariadi.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, Dkt.Fredrick Mlekwa
akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na
Shirika la Kikristo la Life Ministry kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa
Simiyu, mjini Bariadi.
Mkurugenzi
wa Life Ministry hapa nchini, Dismas Shekalaghe wakati wa makabidhiano
ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika hilo la Kikristo kwa Hospitali
Teule ya Mkoa wa Simiyu, mjini Bariadi.
Baadhi
ya Viti vya kubebea wagonjwa(wheel chairs) vilivyotolewa na Shirika la
Madhehebu ya Kikristo la Life Ministry kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa
Simiyu, mjini Bariadi.
No comments:
Post a Comment