Mhandisi
wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya
Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya kifaa cha kupima mvua kwa
Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea vituo hivyo
vinavyotekelezwa na Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na
Mifumo ya Tahadhari uliopo Lushoto Mkoani Tanga Juni 6, 2017.
Mhasibu
Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Consolata Mazigo akiuliza swali kwa
Mhandisi wa mitambo ya hali ya hewa Bw. Michael Minja wakati wa ukaguzi
wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo
ya Tahadhari wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 6, 2017 Lushoto Tanga.
Mhandisi
wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya
Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya mtambo wa kisasa wa usomaji
wa taarifa za hali ya hewa kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
(hawapo pichani) wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha
Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari ulio chini ya Ofisi
hiyo.
Baadhi
ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakinukuu maelezo ya Fundi Sanifu
Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso (hayupo pichani) wakati wa
mkutano wa kutathimini Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za
Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi
hiyo Kilimanjaro, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera
na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Moshi Juni 7, 2017.
Fundi
Sanifu Mkuu Bonde la Mto Pangani Bw. Vendelin Basso akiwasilisha
utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya
Tahadhari kwa upande wa Bonde la Mto Pangani mkoani Kilimanjaro wakati
wa ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi huo uliofanywa na Ofisi ya Waziri
Mkuu Juni 7, 2017.
Mratibu
Taifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya
Tahadhari Bw.Daniel Alfei akiwasilisha mada yake wakati wa mkutano wa
kutathimini Utekelezaji wa mradi huo kwa upande wa Bonde la Mto Pangani
Mkoani Kilimanjaro Juni 7, 2017.
Fundi
Sanifu Hydrojia kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw.Paul Damian
akimuonesha Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri
Mkuu Bi. Grace Moshi kifaa cha kusafirisha taarifa za kuongezeka au
kupungua kwa maji mtoni (Intelligent Top Cap) wakati wa tathimini ya
utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya
Tahadhari Juni 7, 2017 Mkoani Kilimanjaro.
Watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiangalia namna ya Kifaa cha kupima joto
Ardhi (Themometer) ikiwa ni moja ya kifaa kilichofungwa katika
Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya
Tahadhari eneo la Lyamungu Wilayani Hai.
Msaidizi
wa masuala ya Hali ya Hewa Bw. Mbaraka Shaghira (katikati) akieleza
matumizi ya Kifaa cha kupima upepo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu walipotembelea Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na
Mifumo ya Tahadhari ili kuona Utekelezaji wake eneo la Kituo cha Tafiti
cha Lyamungu Wilayani Hai.
Fundi
Sanifu Mkuu Bonde la mto Pangani Bw. Vendelin Basso akionesha namna ya
kusoma kifaa cha kupima kina cha maji kwa Mchumi Idara ya Sera na
Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Bivelyne Muchumbuzi kilichopo katika
Mto Malala wakati wa ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha
Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari chini ya Ofisi hiyo Juni
7, 2017
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment