Rais
mstaafu wa awamu ya nne dk .Jakaya Kikwete akishika Mwenge wa Uhuru
uliopita kutembelea shamba lake la mananasi lililopo Bago -Kiwangwa
Bagamoyo .(Picha na Mwamvua Mwinyi.
Rais
mstaafu wa awamu ya nne dk .Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete
wakikimbiza Mwenge wa Uhuru uliopita kutembelea shamba lake la mananasi
lililopo Bago -Kiwangwa Bagamoyo .
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa Amor Hamad ,akizungumza baada ya kupata
taarifa ya ujenzi ,wa kiwanda cha kusindika matunda cha sayona kilichopo
Mboga – Msoga Chalinze ,kutoka kwa afisa uhusiano wa kampuni mama ya
MMI ,Abubakar Mlawa
………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
RAIS
mstaafu wa awamu ya Nne ambae pia ni mkulima wa tunda la mnanasi
,dk.Jakaya Kikwete,amewataka wamiliki wa viwanda vya matunda kuacha
kuwakandamiza wakulima kwa kununua matunda kwa gharama ya chini .
Amesema
viwanda hivyo vinasaidia kupatikana kwa masoko ya ndani lakini vimekuwa
havina uwiano wa gharama zinazolingana na maumivu anayoyapata
mkulima.Aidha dk. Kikwete ameeleza kumekuwa na changamoto ya kushuka kwa
soko kwa wakati mwingine hali inayokuwa ikisababisha wakulima kupata
hasara kwa matunda kuoza yakiwa mashambani .
Akitoa
taarifa ya shamba lake la mananasi lililipo Bago-Kiwangwa wilayani
Bagamoyo ,wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda kutembelea shamba hilo
,alisema kilimo cha matunda kina tija endapo utalima kisasa na kuwa na
soko la uhakika .
Kikwete
alieleza ,viwanda vya usindikaji matunda mbalimbali ,vinapaswa kumjali
mkulima ambae amekuwa akipata shida na kutumia gharama kubwa kuandaa
shamba .“Wakati utafika watakosa matunda ,kutokana na gharama yao
hailipi ,wakulima wa matunda tushindwa kukubali kuuza kwa bei ya chini
ambayo hailipi ” alifafanua .
Rais
huyo mstaafu ,alimwambia kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2017 ,Amor
Hamad Amor ,kuwa mananasi huvunwa baada ya miezi 18 tangu kupandwa .“Bei
ya mauzo hutegemea wanunuzi na wachuuzi wadogowadogo ambao hununua kwa
ukubwa wa nanasi sh 400 hadi 800 inapovunwa kutoka shambani .
Dk.Kikwete
alisema ,shamba lake lina ukubwa wa hekari 200 ambapo hekar 64 ndizo
zimelimwa na zipo kwenye hatua ya palizi .Alisema pia wana chama chao
cha wakulima wa matunda Kiwangwa wana ambapo wanamatayarisho ya miche
mipya ya kuweza kuuzika nje za nchi.
“Mwenge
kwa kuangaza shambani kwangu ni ishara ya nuru ,basi nitapata neema
baadae,nashukuru kwa kuja kutembelea shamba langu kujionea shughuli
nazofanya baada ya kustaafu” alisema .Kiongozi huyo pia alipita kujionea
shughuli za ujenzi wa kiwanda cha Sayona kinachomilikiwa na kampuni
MAMA ya MMI steel,kilichopo kata ya Mboga.
Afisa
uhusiano wa kampuni za MMI steel ikiwemo Sayona,Abubakar Mlawa
,alimwambia kwamba ,kiwanda cha Sayona kimefikia asilimia 70 ya ujenzi
na mwezi novemba mwaka huu kinatarajia kuanza kazi.Alieleza kiwanda
hicho,kwasasa kimeajiri watu 100 wakiwemo mafundi ujenzi na kitakapoanza
kazi kitaajiri watu 800.
Mlawa
alisema,mahitaji makubwa ni matunda zaidi ya tani tisa kwa siku, hasa
maembe,nyanya na matunda mengine hivyo wakulima wa matunda wachangamkie
fursa hiyo.Alisema kiwanda cha Sayona ni moja ya uwekezaji mkubwa mkoani
Pwani,na kinalenga kugharimu dollar mil.55 sawa na sh.bil.120 katika
ujenzi wake.
Nae
kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Amor Hamad ,alipongeza serikali kwa
kuondoa ushuru wa mazao ya matunda na kuongeza kodi kwa bidhaa
zinazotoka nje ya nchi hali inayoonyesha taifa kutaka kukuza soko la
ndani.Alimpongeza rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Kikwete na kuwataka
wakulima wa zao hilo kuiga mfano wake wa kulima kwa tija .
Amor
aliwataka wananchi kujishughulisha kwa kufuata nyayo za waasisi wetu
akiwemo Kikwete na waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda .“Niipongeze
serikali kwa jitihada hizo kwani inaonyesha serikali inataka kukuza soko
la ndani la nchi na wakulima kuthaminika ili kujiletea maendeleo.
Mwenge wa Uhuru june 10,unatarajia kukabidhiwa mkoani Morogoro ,ukiwa Chalinze na Bagamoyo umepitia miradi iliyogharimu bil.128
No comments:
Post a Comment