Rais Trump na James Comey |
Kamati ya Bunge la Seneti la masuala ya
usalama nchini Marekani imechapisha ushahidi utakaotolewa na mkurugenzi
aliyetimuliwa kazi FBI ambaye amesema Rais Trump alimtaka mkurugenzi
huyo kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama.
James Comey alitoa uchambuzi wa ushaidi
wa mazungumzo kati yake na rais Trump aliyofanya naye mara tano wakati
Trump alipokuwa akirudia kutaka amsikilize na kumheshimu wakati ambapo
Comey anasema alikuwa akifanya kazi zake bila kuegemea upande wowote.
- Trump amuonya mkuu wa FBI aliyefutwa James Comey
- James Comey anadaiwa kukataa kumtii rais Trump
- Trump atetea hatua ya kumfuta Comey
Wakili wa Trump amesema rais Trump
anahisi kuna ukweli kwa uthibitisho kuwa yeye mwenyewe binafsi hakuwa
akichunguzwa kwa timu yake ya kampeni zake kuhusishwa na Urusi.
Maafisa wawili wanaohusika na
usalama,Mike Rogers na Dan Coats wamewaambia maseneta kuwa hawakuwahi
kulazimishwa kufanya jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria
No comments:
Post a Comment