Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema tatizo la kuharibika kwa mashine
ya kusagia taka katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja siku za karibuni
kulipelekea kurundikana kwa taka na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Amesema
baadhi ya wafanyakazi wakorofi wa Hospitali hiyo walitumia kasoro hiyo
kuzitupa taka kwenye ufukwe wa bahari, nyuma ya Hospitali, ambapo ni
kosa kwa mujibu wa sheria na kanuni za afya na uhifadhi wa mazingira.
Waziri
Mahmoud ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea mashine ya
kusagia taka zinazozalishwa katika Hospitali hiyo ambayo hivi sasa
imefanyiwa matengenezo na ipo tayari kufanyakazi na kuondosha kero hilo.
Amesema
wafanyakazi saba waliobainika kufanya kosa la kutupa taka sehemu ya
ufukwe wamechukuliwa hatua za nidhamu na kuuagiza uongozi wa Hospitali
ya Mnazimmoja kutomvumilia mfanyakazi atakaekiuka kanuni za afya.
Hata
hivyo Waziri wa Afya amekiri kuwa uzalishaji wa taka katika Hospitali
ya Mnazimmoja umekuwa mkubwa kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa
baada ya kutanuliwa na kufikia daraja la kuwa Hospitali ya rufaa.
Ameyashauri
Makampuni yanayohitaji taka kwa ajili ya kuzisarifu na kuzigeuza kwa
ajili ya matumizi mengine waonane na uongozi wa Hospitali kwani sehemu
kubwa ya taka hizo zinaweza kutumika kwa shughuli nyengine.
Amesema
hivi sasa uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja umeandaa utaratibu mzuri
wa kukusanya taka ambapo za aina moja zinatiwa katika pipa moja na
mapipa hayo yamewekwa katika wodi ili kuondosha usumbufu kwa
wafanyakazi, wagonjwa na watu wanaofika kwa shughuli mbali mbali.
“Nataka
wananchi wawe waangalifu wakati wa kuhifadhi taka kwani kila pipa
linatiwa taka maalumu na hakuna kuchanganya taka zote katika pipa moja,”
alisisitiza Waziri Mahmoud.
Amewataka
wafanyakazi wa Hospitali kusimamia na kuwaelimisha wananchi matumizi ya
mapipa hayo ili kila pipa liingizwe taka zinazostahiki ili kuondosha
usumbufu wakati wa zoezi la kuzisaga.
Mtaalamu
wa mashine ya kusagia taka kutoka Kenya Benard Abere amemueleza Waziri
wa Afya kwamba kazi ya kuifanyia matengenezo mashine hiyo imekamilika na
katika kipindi cha wiki moja mkusanyiko wa taka utaondoka.
Waziri
wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipata maelezo ya mashine
mpya ya kusagia taka za hospitali kwa Mtaalamu wa mashine hizo kutoka
Kenya Benard Abere. Picha na Makame Mshenga.
No comments:
Post a Comment