Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Uongozi
wa Klabu ya Simba, umeweka bayana uamuzi wao wa kwenda Shirikisho la
Soka la Kimataifa (Fifa) kudai haki yao baada ya kupokwa pointi tatu na
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji huku wakiwa wanasubiri
barua kutoka Bodi ya Ligi ili wawasilishe malalamiko yao.
Simba
imefikia hatua hiyo baada ya Kamati ya utendaji kukaa na kuamua kwa
kauli moja kulipeleka mbele zaidi suala hilo kutokana na kuona kasoro za
kikanuni katika maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa
Usimamizi wa Ligi kwa sababu ambazo wanaziona si za msingi kutokana na
kanuni kuwa wazi.
Akizugumza
na wanahabari leo Jijini Dar es salaam, Rais wa klabu ya Simba, Evans
Aveva, amesema wanachokisubiria kwa sasa ni ku njia zipo nyingi za wao
kupata haki yao, hivyo wanasubiri kupewa barua kutoka Bodi ya Ligi
ambayo wataiambatanisha kwenda Fifa kudai haki yao.
Aveva
amesema wamefuatilia njia za kudai haki yaona wameambiwa gharama
inaweza kuanzia dola 15,000 na wapo tayari kulipa ili tupate haki yao
ambayo mpaka sasa wanasikia tu kama wamepokwa pointi 3 walizopatiwa na
kamati ya saa 72 baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar
ambayo inadaiwa ilimchezesha beki wake, Mohammed Fakhi akiwa na kadi
tatu za njano dhidi yao.
Maazimio
hayo yaliyofikiwa kwa pamoja na kamati ya utendaji yameainisha kuwa
pamoja na hilo, pia wanapeleka malalamiko yao kuhusiana na mchezaji wao
Mbaraka Yusuph aliyeidhinishwa kucheza katika klabu ya Kagera wakati
tayari akiwa na leseni ya kuchezea ya klabu ya Simkba.
"tunafahamu
kuwa TFF wanakuwa ni wazito katika kusikiliza masuala au malalamiko ya
klabu yetu ya Simba, tukianzia na kesi ya Singano, mchezaji Mbaraka
Yusuph ambaye anacheza Kagera kwa sasa wakati wao kama Shirikisho
walitoa leseni ya mchezaji huyo kwetu sisi na kila kitu kipo wazi
kabisa,"amesema Aveva.
Mbali
na hilo, Aveva uamuzi wa Rais wa TFF kupeleka fainali Jamhuri Dodoma
wala hatuwezi kuupinga kwani Simba imejiandaa kucheza fainali sehemu
yoyote kwani hakuna wa kuizuia pale inapotaka jambo lake.
Aveva
ametoa kauli hiyo baada ya jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kupitia kwa rais wake, Jamal Malinzi kutangaza mechi ya fainali ya FA
kati ya Simba na Mbao itapigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
"sisi
hatuidharau Mbao, ila hatuiogopi kwani ni timu ndogo na hata katika
mkoa wa Dodoma tuna mashabiki wengi sana tunachotaka kuwaambia kuwa
fainali tutacheza kokote,"amesema Aveva.
Raisi
wa Klabu ya Simba Evance Aveva akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na uamuzi wa kamati ya Utendaji wa klabu hiyo kuazimia kwa
pamoja kupeleka malalamiko yao Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA
kutokana na kutokufa nyiwa haki na Shirikisho la Mpiera wa Miguu Nchini
TFF.
Raisi wa Klabu ya Simba Evance Aveva akionesha leseni ya mchezaji Mbaraka Yusuph waliyopatiwa na Shirikisho la Mpiera wa Miguu Nchini TFF,
No comments:
Post a Comment