Washiriki
wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kukabidhiwa mikopo ya riba nafuu toka
Jiji la Arusha.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa
Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro amesema wanawake na vijana wanaokidhi
vigezo wapewe Zabuni za Halmashauri ya Jiji ili kuweza kuwainua kiuchumi na
kuboresha maisha yao kwa kazi mbalimbali zinazotolewa kila mwaka.
Daqarro
ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wanawake na vijana ambao ni
wajasiriamali wanaonufaika na mikopo yenye riba nafuu kutoka Jiji ambayo
hutolewa kwa mujibu wa sheria.
“Ni wakati wa wanawake na vijana kuchangamkia
fursa mbalimbali katika Jiji la Arusha ikiwa ni pamoja na zabuni ambazo
zitasaidia kuinua mitaji na kuongeza pato la familia zenu, hizi kazi ni zenu
hakikisheni mnafuata taratibu zote ili mzichukue wasije watu toka mbali wakapewa
wakati ninyi ambao ni wakazi wa Mji huu mkakosa kwa kukosa vigezo vidogo
watumieni wataalamu wa Jiji wawaelimishe”amesema Daqqaro.
Wakati
akisema hayo Mkuu wa Wilaya, Daqarro
amekabidhi hundi za mfano ya Tsh Mil 390 kwa vikundi vya wanawake 78 huku
vikundi vya vijana 67 vimekabidhiwa hundi ya Tsh Mil 336.
Daqarro amesema kuwa kutokana na changamoto
iliyoko katika taasisi za fedha ambazo hutoa mikopo kwa riba kubwa na kuhitaji
dhamana ya nyumba na ardhi jambo ambalo linawakwamisha wakopaji hivyo Serikali imeamua
kutoa mikopo ya masharti nafuu ambayo ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya
Halmashauri.
Pia
amewasihi wanufaika wa mikopo hii kuwa mikopo itumike katika malengo maalumu na
katika miradi inatakayoleta tija kama vile uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo
ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kukuza uchumi.
Kwa upande
wao kinamama na vijana waliopokea mikopo hiyo wamesema kuwa mikopo hiyo
itawainua kiuchumi na kuwawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali na
kuachana na kuwa tegemezi pamoja na matumizi ya dawa za kulevya na wizi.
Mpaka
kufikia robo ya tatu Machi 2017 Halmashauri ya jiji la Arusha imetoa mikopo ya Tsh
Bil 1.3 kwa ajili ya wanawake na
vijana kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
|
No comments:
Post a Comment