Na Veronica Simba - Arusha
Jumla
ya wanawake 18 kutoka mikoa mbalimbali nchini, jana (Mei 19, 2017)
wamehitimu mafunzo ya ukataji na ung'arishaji madini ya vito katika
Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini Arusha.
Wahitimu hao wa awamu ya nne, wamefanya idadi ya waliohitimu tangu kuanzishwa mafunzo husika katika Kituo hicho kufikia 65.
Akizungumza
katika sherehe za Mahafali hayo, Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, alitoa
wito kwa wadau wa madini ya vito nchini, kuwapa ajira na ushauri wa
kitaalam wahitimu, ili waweze kujiajiri katika shughuli za uongezaji
thamani madini.
"Lengo ni kuhakikisha kuwa ukataji unafanyika kwa viwango vya kimataifa ili kuweza kuuza zetu kwenye masoko ya nje."
Aidha,
Dkt. Pallangyo alitoa changamoto kwa wadau wote wa madini ya vito
kuendelea kukuza shughuli za uongezaji thamani madini kwa kubadilishana
uzoefu na wakataji wa madini ya vito mahiri duniani.
"Kwa
wale wafanyabiashara wa madini ya vito, mlioajiri wataalam wa kigen,
natoa rai muendelee kuwahimiza watoe mafunzo kwa watanzania wanaofanya
nao kazi, ili kuhawilisha utaalam huu adimu," alisisitiza.
Vilevile,
Naibu Katibu Mkuu, aliwaasa wahitimu kuwa mabalozi wazuri wa Kituo
kinachotoa mafunzo hayo ya TGC, kwa kuendelea kufanya shughuli za
uongezaji thamani madini popote watakapokwenda.
Alitoa
rai kwa uongozi wa TGC kujenga utamaduni wa kuwaalika wahitimu wote wa
Kituo hicho hususan waliojiajiri, kushiriki katika sherehe za Mahafali,
ili waoneshe bidhaa zao.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka,
akitoa historia ya TGC, alisema kuwa, Wizara ya Nishati na Madini
iliamua kuwekeza katika Kituo hicho kwa malengo ya kutoa mafunzo ya
kuongeza thamani madini ya vito kwa wachimbaji wadogo na wajasiriamali
wa madini hayo.
Aliongeza
kuwa, malengo mengine ni pamoja na kukuza na kufanikisha shughuli za
uongezaji thamani katika madini ya vito nchini, kukuza na kuendeleza
ujuzi na ufahamu wa kutambua madini ya vito na kuongeza kipato na ajira
kwa watanzania.
Alisema
kuwa, katika kujenga uwezo wa ndani na kupata wakufunzi wenye sifa za
kimataifa; Wizara ilipeleka watumishi watatu nje ya nchi kujifunza
masomo ya vito na usonara kwa lengo la kuwa wakufunzi katika Kituo
hicho. "Watumishi hao walikwishahitimu mafunzo yao na tayari
wamesharipoti kituoni."
Mhandisi
Mchwampaka alisema kuwa, Wizara inakusudia kupeleka watumishi wengine
watano nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo husika ili kukijengea uwezo
Kituo kwa kuwa na walimu wa kutosha.
Akizungumzia
mafunzo mengine yanayotarajiwa kutolewa na Kituo hicho baadaye, alisema
kuwa ni pamoja na Jemolojia, Utengenezaji wa bidhaa za mapambo pamoja
na uchongaji wa vinyago vya mawe.
"Aidha, Kituo kitaanzisha maabara ya utambuzi na uthibitishaji wa madini ya vito na bidhaa za urembo.
Akisoma
risala mbele ya Mgeni Rasmi, kwa niaba ya wahitimu wenzake, Theresia
Mollel, alisema kuwa mafunzo hayo yamewapa uwezo kama wanawake wa
kufanya kazi katika sekta ambayo wengi hudhani wanawake hawaiwezi.
"Kupitia
mafunzo haya, tunaihakikishia jamii kuwa wanawake tunaweza kufanya
mabadiliko katika tasnia ya madini ya vito na kuleta maendeleo katika
jamii na Taifa kwa ujumla."
Kituo cha Tanzania Gemological Centre (TGC) kilianzishwa mwaka 2003.
Mafunzo haya hutolewa kwa muda wa miezi saba ambapo miezi sita ni nadharia (darasani) na mwezi mmoja ni mafunzo kwa vitendo.
Wanafunzi
hawa wanafadhiliwa na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Kamati ya
Maonesho ya Madini ya Vito ya Arusha (Arusha Gem Fair) chini ya Mfuko wa
Kuwaendeleza Wanawake.
Mgeni Rasmi, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
(mwenye koti la mauamaua), akikagua kazi za uongezaji thamani madini ya vito,
zinazofanywa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini
Arusha.
Mgeni Rasmi, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
(mwenye koti la mauamaua), akikagua kazi za uongezaji thamani madini ya vito,
zinazofanywa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini
Arusha.
Wahitimu wa mafunzo
ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia
Tanzania (TGC), wakiwa darasani.
Wahitimu wa mafunzo
ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia
Tanzania (TGC), wakiwa darasani.
Wahitimu wa mafunzo
ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia
Tanzania (TGC), wakiwa darasani.
Wahitimu wa mafunzo
ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia
Tanzania (TGC), wakiwa darasani.
Mgeni Rasmi, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
(mwenye koti la mauamaua), akijumuika pamoja na wahitimu wa Kituo cha Jemolojia
Tanzania (TGC) kucheza muziki.
Kamishna wa Madini
Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, akisoma historia ya Kituo cha Jemolojia
Tanzania (TGC), kwa Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
Mgeni Rasmi katika
sherehe za mahafali ya Nne ya Mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito
nchini, Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (mwenye koti la mauamaua – walioketi) na Kamishna wa Madini Tanzania,
Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na
wahitimu.
Mwanafunzi bora,
Happiness Ernest, akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni rasmi.
No comments:
Post a Comment