Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI
wilaya ya kilolo mkoa wa Iringa imewataka wananchi wa wilaya
hiyo wanaojishughulisha na kilimo cha mazao mbali mbali kuacha
kuuza mazao yao kwa vipimo visivyo sahihi marufu kwa jina la
Lumbesa na badala yake kuuza mazao kwa kutumia vipimo sahihi kama
mizani .
Akiwahutubia
wananchi wa kijiji cha Irindi na Magana kata ya Mahenge wilayani
Kilolo mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdala leo wakati wa
ziara yake ya kukagua miundo mbinu ya elimu na uhamasishaji
wananchi kushiriki shughuli za uzalishaji mali ,mkuu huyo alisema
kuwa iwapo wananchi hao watakubali kuuza mazao yao kwa ujazo batili
hatua kali itachukuliwa kwa muuzaji na mununuzi .
Hivyo
aliwataka viongozi wa serikali za vijiji na kata zote
kuwasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa faida na kuwabana
walanguzi wa mazao wanaowapunja wakulima hao kwa kununua mazao kwa
vipimo ambavyo vinawanyonya wakulima.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa wilaya hiyo imejaliwa kwa kuwa na
ardhi nzuri inayokubali mazao ya kila aina kama vitunguu,mahindi
,maharage ,njegere ,nyanya na mazao mengine mengi hivyo jukumu
kubwa la mabwana shamba ni kuwasimamia wakulima hao dhidi ya
walanguzi wa mazao yao na kuona kila mkulima ananufaika na kilimo
na sio kuishia kuwanufaisha wafanyabiashara .
Alisema
kuwa chini ya serikali ya Rais Dkt John Magufuli serikali
inayowajali wananchi wake wote pasipo kuwabagua asingependa kuona
Kilolo wafanyabiashara wakiwanyonya wakulima na kuwa kama
walizoea kipindi kabla ya Dkt Magufuli hajaingia Ikulu basi ni
vema watambue kuwa mwisho wa mkulima Kilolo kumnufaisha
mfanyabiashara ama dalali wa mazao mwisho wake ulikuwa ni mwaka
2015 ila serikali hii ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya
watanzania wote .
Hivyo
aliwataka wakulima wilaya ya Kilolo kuuza mazao yao kwa
utaratibu na kwa kuzingatia vipimo sahihi vinavyotambuliwa na
serikali na sio vinginevyo .
Meneja wa vipimo mkoa wa Iringa Zainabu Kafungo aliwaeleza
wananchi hao kuwa kutokana na elimu mbali mbali ambayo imeendelea
kutolewa na ofisi yake na viongozi wa serikali mkoani Iringa kasi
ya wananchi kuuza mazao yao kwa vipimo visivyo sahihi imeendelea
kupungua na hata wafanyabiashara hasa madalali wa mazao
wameendelea kuogopa kuwaibia wakulima .
Alisema
kuwa ofisi yake ni wakala wa serikali inayosimamia vipimo vyote
nchini Tanzania bara lengo ni kuhakikisha kunakuwepo na usahihi wa
bidhaa zinazofungashwa kwa ajili ya kumlinda mlaji asipunjwe
kutokana na vipimo apate huduma kulingana na pesa yake .
Pia
kumlinda mlaji kwa kufanya kaguzi za bidhaa zilizofungashwa
mashambani toka kwa wakulima kuwa zinakuwa kwenye vipimo sahihi na
sio lumbesa
Aidha alisema ufungashaji batili ni ufungashaji kinyume na sheria ya
vipimo sura 340 mapitio ya mwaka 2002 pamoja na kanuni zake japo
alisema kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya viongozi maeneo
kuhamasisha wananchi kutotii sheria na baadhi ya taasisi kuandaa
kanuni zao bila kurejea sheria ya vipimo .
Sheria
inataka kiasi cha ufungashaji kwa uwele ,karanga ,ufuta,wimbi
,mtama ,maharage na jamii yake kilo 90 tu wakati alizeti kilo
40,mkaa kilo 30, viazi ,mazao mengine ambayo hayajatajwa ni kilo
100,korosho kilo 80 na kuwa faini mbali mbali zipo wazi kwa
wakiukwaji wa sheria kwa Yule atakayekiuka sheria ya vipimo
hufikishwa mahakamani faini yake si chini ya 300,00 na si zaidi ya
shilingi 50,000,000 au kifungo kisichozidi miwiliau vyote kwa pamoja
.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah akiwataka wananchi wa kijiji cha Irindi na Magana kata ya Mahenge kuachana na uuzaji mazao kwa vipimo batili |
Wananchi wa wakiendelea kusoma vipeperushi vya elimu sahihi ya vipimo wakati mkutano wa DC ukiendelea |
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akiwahutubia wananchi mwenye kilembe cha madoa mekundu ni meneja wa vipimo mkoa wa Iringa Zainabu Kafungo. |
No comments:
Post a Comment