Mkulima
mmoja Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo (31)anashikiliwa
na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kukutwa na sare na vifaa vingine vya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) ambavyo anatuhumiwa kuvitumia
kupateli na kuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka kwa vijana
wanaotafuta nafasi ya kujiunga na Jeshi hilo.
Taarifa
hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Mkoa wa Tabaora Wilbroad Mtafungwa
alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Ofisi kwake juu ya hatua
mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.
Alisema
kuwa Polisi walifanikiwa kumukamata mtuhumiwa huyo katika Hoteli ya JM
iliyopo Wilayani Igunga akiwa na sare mbalimbali za Jeshi la waananchi
Tanzania (JWTZ) zikiwa na cheo cha Koplo ambavyo ni pamoja na kofia
tatu, begi, sweta, buti jozi moja, magwanda na mikanda mitatu.
Mali
nyingine zilikamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni pamoja na fomu za likizo cha
likizo , fomu za kujaza vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hilo na Jeshi
la Kujenga Taifa(JKT) kwa mujibu wa Sheria na hiari na mihuli zenye
nembo inayofanana na Jeshi hilo.
Kamanda
Mtafungwa alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia nyaraka na sare za
Jeshi hilo kuchukua fedha kwa kuwadanganya na kuwatapeli wananchi
mbalimbali kwa kudai atawatafutia ajira katika majeshi ya Kujenga Taifa
na la Wananchi.
Kamanda
huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo pia alikutwa barua
kutoka Serikali za mitaa za Dar es salaam na gari aina ya Toyota
Starlet yenye namba za Usajili T633 ARF ambalo wanaendelea kuchunguza
uhalali wa umiliki wake na ambalo mtuhumiwa alikuwa akilitumia na
kuwafanya baadhi ya wananchi wamuamini kuwa atawasaidia kupata nafasi
katika majeshi.
Aliongeza
kuwa mtuhimiwa huyo pia alikuwa na barua za maombi ya watu ya kuomba
kujiunga na Jeshi, Fomu za Matibabu za Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na
nakala ya Vyeti vya kumaliza elimu ya Sekondari vya baadhi ya watu.
Kufuatia
tukio hilo alitoa wito kwa waananchi waliowahi kutapeli ndani na nje ya
Mkoa wa Tabora kujitokeza katika vituo vya Polisi ili waweze kutoa
ushahidi utakasaidia kuonyesha ni jinsi gani walivyumizwa na mtuhumiwa
huyo .
Kamanda
Mtafungwa alisema kuwa Polisi inaendelea kushirikiana na JWTZ ili iweze
kubaini sare na vifaa hivyo alivipata wapi , kwa lengo lipi na ni nani
aliyompatia ili wahusika wote waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria
kwa hatua zaidi.
Aidha ,
Kamanda huyo aliwaasa wananchi kuwa makini na matapeli wanaowadai fedha
na kuwadanganya kuwa watawatafutia kazi katika Majeshi kwani vyombo
hivyo vinaotaratibu wake ambao ndio unaotumika kuwapata vijana
wanaojiunga kwa mujibu wa sheria na wale wa hiari na sio kwa
kuchangishwa fedha.
Wakati
huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kukamata watuhimiwa
17 kwa kukutwa na lita 205.25 za gongo wakati wa msako wa kukamata wa
watumiaji na wauzaji wa bidhaa hizo haramu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Mtafungwa alisema kuwa watuhimiwa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao wakati wowote.
Aidha ,
alisema kuwa katika zoezi hilo pia Polisi ilifanikiwa kuteketeza ekari
tano na nusu za mashamba ya zikiwa na uzito wa kilogramu 220 yalikuwa
yamelimwa katika Msitu wa Hifadhi wa Igombe wilayani Uyui.
Alisema
kuwa jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mashamba hayo zinaendelea na
kuwaomba wananchi wenye taarifa ya walipo wahusika walisaidie Jeshi la
Polisi ili wahusika waweze kufikishwa Mahakama kujibu tuhuma zao
No comments:
Post a Comment