Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetakiwa
kuhakikisha kwamba wanatumia vyema kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan
katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na uwezo mkubwa katika tiba
mtandao.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha ya
siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo.
Warsha
hiyo ilikuwa inakokotoa tiba mtandao ili kuwezesha mradi wa majaribio
wa Tiba mtandao unaohusisha wadau mbalimbali kutekelezwa. Kitovu cha
mradi huo ni kijiji cha Ololosokwan kilichopo Waso wilayani Ngorongoro.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk
Mpoki Ulisubisya akizungumza na wataalamu kutoka KCMC, MUHAS wadau
kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi,
Bill & Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa
mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya
siku mbili ya tiba mtandao iliyofanyika MUHAS jijini Dar es
Salaam.(Picha zote na Thebeauty.co.tz)
Katibu
huyo alisema kutumia kikamilifu kwa kijiji hicho hakumaanishi kuwa na
majengo bali kutumia kufunza wataalamu mbalimbali kutokana na ukweli
kuwa kijiji hicho sasa kitakuwa mfano wa utendaji katika kusaidia
wananchi wa Tanzania.
“Uwapo
wa kijiji hiki ni tukio kubwa kwetu kwani ni kijiji cha kujifunzia,
namna ya kutibu, namna ya kukusanya takwimu namna ya kubaini mahitaji na
… ni mfano wa namna gani teknolojia inaweza kufanya mambo makubwa”
alisema Ulisubisya .
Alisema
yeye anaamini kwamba si lazima wataalamu watiba wafundishwe eneo moja,
kama ilivyo sasa, lakini wanaweza kufundishwa katika eneo kama
Ololosokwan na hivyo kuwajenga pia kisaikolojia kwamba wanaweza
kufanyakazi pembezoni bila ya tatizo.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues (kushoto) akichangia jambo wakati wa kuhitimisha
warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. Wa pili
kushoto ni mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Ephata Kaaya (wa
pili kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia).
Alisema
mafanikio ya dhana ya tiba mtandao yatasaidia sana kuboresha hali ya
watanzania kwa kuwa mahitaji yao yatajulikana mapema na kutokana na
ukweli kuwa mradi wenyewe unahusisha pia ukusanyaji wa data wa uhakika
kwa kuzingatia mahudhurio ya watu na magonjwa yao.
Pia
alisema kwa utekelezaji thabiti utaonesha namna ambavyo Watanzania tuko
mbele na kusema kwamba mradi huo wa tiba mtandao anauelewa na
ameupigania sana nje ya nchi ambako amekwenda kuzungumza.
“Mwaka
jana mwezi Desemba nilienda kwenye mkutano Washington unaohusu Tiba
mtandao na tumeuza sana hili wazo la tiba mtandao kwa wenzetu, kwa hiyo
watakuja kujifunza tunafanyaje” alisema Dk. Ulisubisya na kuongeza
kwamba Wizara yake itatoa ushirikiano wa kutosha kuona dhana hiyo
inatekelezeka tena kwa ufanisi.
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi - Muhimbili
(MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) akitoa maoni wakati wa kufunga
warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo.
Kwa
mujibu wa mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa
majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu na
kutanuka kwa jinsi inavyowezekana kwa kuangalia ufanisi wa kijiji.
“Dhana
hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye
ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi
huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,” alisema Zulmira
Tiba
mtandao katika kijiji hicho itahusisha upasuaji mdogo ambao utafanywa
na watendaji waliopo katika kliniki za kijiji hicho wakielekezwa na
mtaalamu bingwa.
Mhadhiri
na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Tehama wa Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi - Muhimbili (MUHAS), Felix Sukums akiwasilisha
mapendekezo ya mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao kwa mgeni
rasmi (hayupo pichani), Kushoto ni Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali
kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen.
Aidha
akizungumza katika ufungaji wa warsha hiyo Zulmira alitaka kuwapo kwa
matumizi ya maabara ya kisasa iliyopo hapo ili iweze kusaidia taifa.
Hata
hivyo mwakilishi huyo wa UNESCO alisema kwamba Daktari wa wilaya ambako
kijiji cha Ololosokwan kipo anahitaji kiasi cha dola elfu 70
kukamilisha baadhi ya mambo ili kuwa na uhakika pamoja na kuleta
madaktari wa Afrika mabingwa kuja kufanya kazi kwa muda.
Akizungumzia
suala hilo, Dk Ulisubisya alisema kwamba anajua shida iliyopo, lakini
akamwagiza DMO kukaa na DAS (Katibu Tawala Ngorongoro) kuona namna ya
kufanikisha haja ya sasa ya nyumba za makazi kwa gharama nafuu na kusema
anaamini wanaofaidika wako tayari kusaidia kidogo.
Alisema bajeti hiyo naamini inaweza kupungua kwa kutumia mali ghafi rahisi yenye kudumu zaidi.
Majadiliano
yakiendelea katika kuboresha mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba
mtandao wa kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha
wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya siku 2 iliyofanyika MUHAS.
Pia
aliwashukuru UNESCO kwa kuwezesha Ololosokwan kuwa sehemu ya kujifunza
na kutanua mradi wa tiba mtandao ambao amesema kwa kuzingatia teknolojia
iliyopo sasa Watanzania na dunia kwa ujumla wanapata nafasi ya tiba
bila kuwa karibu na bingwa.
Katika
utekelezaji wa mradi huo hatua ya pili mifumo yote (maunganisho ya
kisetelaiti) inatarajiwa kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na
nafasi ya kuanza matibabu ifikapo Oktoba mwaka huu au mapema zaidi.
Mradi
huo unoanza kwa majaribio unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika
kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwani na kwa
kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa,
masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza
kufanya tiba kwa kutumia mtandao.
Mratibu
wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akifafanua jambo kwa mgeni
rasmi wakati wa kuhitimisha warsha hiyo.
Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mwezi Novemba mwaka 2016.
Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo.
Warsha
hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari kutoka
Arusha , Manyara , Kilimanjaro na Dar es salaam ilichambua dhana ya tiba
mtandao na kuidadavua dhana ya utekelezaji kamilifu wa jaribio la
utoaji wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na na namna
ya kuirasimisha kama mfumo wa kuboresha afya maeneo yaliyo pembezoni ya
miji na vijijini.
Mmoja
wa washiriki akiwalisha maoni kwenye warsha ya siku 1 ya kujadili
mapendekezo ya mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao
iliyomalizika MUHAS jijini Dar es Salaam.
Picha
juu na chini wataalamu kutoka KCMC, MUHAS, UNESCO, wadau kutoka The
Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill &
Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa mikoa na
wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili
ya kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao iliyofanyika
MUHAS jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues akimshukuru mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya mara
baada ya kufunga warsha hiyo ya siku 2 iliyofanyika katika kumbi za
MUHAS, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller
(kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues
(katikati) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) baada ya
kuhitimisha warsha ya siku 2 ya mradi wa tiba mtandao iliyofanyika
jijini Dar es Salaa., MUHAS.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya katika picha ya pamoja na washiriki wa
warsha hiyo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk
Mpoki Ulisubisya akimpongeza Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali
kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen mara baada ya kufunga warsha ya siku 2
iliyofanyika katika kumbi za MUHAS, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment