Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza katika Mkutano
uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu,
Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisaini kitabu cha wageni
Mara baada ya kufika Shule ya Msingi Ubungo Plaza kwa ajili ya Mkutano
uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzAbZ5zMA0kEtEZK240xvUbqLplMQo5F1MZSXkKHGC_1p2KyC0CeQR7gHQLZU2peAPcuCPSzCVsJxLwdw6N0yH0HGQGDjeDpf8j5JAU_0j5_FPnfZYl35KxANAfbdMqpW3Q60-S5MIYtyH/s640/IMG-20170519-WA0322.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8erNj3XrbrhdytXXBF9OIMJzDJV_XczmOIfVTb0tv174scKWsfoGb7kLvvFOXc6xzer4oddjD4r6SssA9YC0FVMLJfmjlpaJxG6FZV0iYsl2SFlX3jqIE2Kjngyt9a7RIvGRHGklXVXPW/s640/IMG-20170519-WA0316.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzAbZ5zMA0kEtEZK240xvUbqLplMQo5F1MZSXkKHGC_1p2KyC0CeQR7gHQLZU2peAPcuCPSzCVsJxLwdw6N0yH0HGQGDjeDpf8j5JAU_0j5_FPnfZYl35KxANAfbdMqpW3Q60-S5MIYtyH/s640/IMG-20170519-WA0322.jpg)
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua Mipaka ya eneo la
Shule ya Msingi Ubungo Plaza kabla ya Mkutano uliofanyika katika Shule
ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa
Mitaa, na wananchi.
Kaimu
Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa Utumishi Mkuu Manispaa ya Ubungo Ndg Ally
Ally akijibu baadhi ya maswali ya wananchi wakati wa Mkutano
uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu,
Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.
Kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally, Katibu Tawala
wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo Na Ofisa Mtendaji wa Kata Ya Ubungo
Ndg Isihaka Waziri wakisikiliza Maelezo kuhusu Shule ya Msingi Ubungo
Plaza kabla ya Mkuu wa Wilaya kuzuru shuleni hapo kwa ajili ya Mkutano![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjL1o5DmJghbvgc10tFhvD7tHsoHke7zlHPkFQnrMnkt_qL78GxkKptHhyjrLTGYZfazVElmOcWiU1-fDPOLC8vs0t-hwf3dbOPLF2OYaowzTJfCQ5nOFTVrJTrEbOcA5XKrj-xA8qAwWxz/s640/IMG-20170519-WA0286.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjL1o5DmJghbvgc10tFhvD7tHsoHke7zlHPkFQnrMnkt_qL78GxkKptHhyjrLTGYZfazVElmOcWiU1-fDPOLC8vs0t-hwf3dbOPLF2OYaowzTJfCQ5nOFTVrJTrEbOcA5XKrj-xA8qAwWxz/s640/IMG-20170519-WA0286.jpg)
Wananchi
wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku
Makori wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza
uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjl-5O9kLJU4A15R2dnc3EPGT-SsO7SjPTN7qxn7GE8kmse7zJ1IQVkQuKrseEfWap_T2oonGY2FsIBQQLLEEP4Zpj3Ae7U9ETx4TZTcrJqlYGU6T4T9Sx0IaZvTHc7QmBzT45hTILrbzV6/s640/IMG-20170519-WA0282.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjl-5O9kLJU4A15R2dnc3EPGT-SsO7SjPTN7qxn7GE8kmse7zJ1IQVkQuKrseEfWap_T2oonGY2FsIBQQLLEEP4Zpj3Ae7U9ETx4TZTcrJqlYGU6T4T9Sx0IaZvTHc7QmBzT45hTILrbzV6/s640/IMG-20170519-WA0282.jpg)
Wananchi
wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku
Makori wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza
uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori ameagiza
kujengwa madarasa nane mapya katika shule ya Msingi Ubungo Plaza Jijini
Dar es salaam kutokana Na uchakavu wa Majengo ya madarasa yaliyopo sasa.
Ametoa
agizo hilo katika mkutano wake na uongozi wa shule hiyo ukiwajumuisha
mtendaji na wajumbe wa mitaa,walimu na wananchi ambao waliohudhuriwa
katika viwanja vya shule ya Msingi Ubungo Plaza.
Mhe
Makori amesema kuwa ili kuboresha elimu katika Wilaya ya Ubungo ni wazi
kuwa ni lazima kuwe Na miundombinu rafiki kwa wanafunzi wanapokuwa
darasani kwa ajili ya masomo kwani ubovu wa Majengo ya shule,ubovu na
uhaba wa vyoo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea wanafunzi kufeli
kutokana na kutokuwa Na miundombinu rafiki.
Alisema
kuwa Kodi zinazokusanywa Na serikali kwa wananchi ni kwa ajili ya
kuwaimarishia miundombinu kuboresha afya, na Elimu hivyo serikali ni
lazima ishughulikie na Kusimamia shughuli zote ikiwemo Ujenzi wa
madarasa kwa manufaa ya wanafunzi Na wananchi kwa ujumla.
Mkuu
wa Wilaya ametoa maagizo hayo Wakati akijibu Risala iliyosomwa Na Mkuu
wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza Bi Theresa Masaba ambayo ilibainisha
changamoto nyingi ikiwemo Ukosefu wa Vyoo Bora, Ukosefu wa Uzio,
Uchakavu wa Majengo ya shule, Upungufu wa Majengo (Ofisi ya Walimu,
Darasa la awali Jiko, Maktaba), Maji taka kuelekezwa kwenye eneo la
shule, Eneo la shule kufanyika kama sehemu ya kuvutia bangi Wakati wa
jioni na siku za Wikendi sambamba na Upungufu wa samani za shule.
Mhe
Mkuu wa wilaya ameagiza pia kuvunjwa kwa Vyoo vilivyopo Na kujengwa
Vyoo vingine vipya sambamba na kujengwa kwa uzio wa shule ili kuepuka
kadhia ya watu wanaotumia kama Eneo la kuvutia bangi Na vitendo vingine
viovu visivyo kubalika katika jamii.
Aidha
amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha anawakamata watu wote
wanajihusisha Na uvutaji bangi katika Eneo la shule kwani Jambo hilo
halikubaliki si tu Na shule hiyo Bali Na serikali kwa ujumla.
Sambamba
Na hayo pia Mkuu wa wilaya ameagiza kuvunjwa kwa ukuta wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) ambapo Uzio wake umejengwa ndani
ya Eneo la shule.
Alisema kuwa Kanisa hilo
tayari lilishapewa Notisi ya siku Saba tangu Mei 8 mwaka huu kwa ajili
ya kuvunja ukuta huo lakini hawakufanya hivyo.
Akitoa
salamu za shukrani kwa niaba ya Walimu Na wanafunzi wa shule,
Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya Msingi Ubungo Plaza Ndg Ramadhani
Maughuu amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutembelea shule hiyo Na
kutatua changamoto hizo zilizokuwa zinaikabili shule hiyo kwa muda
mrefu.
Maughuu
ametoa pongezo zake pia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C.
Makonda kwa ufanisi Na uchapa Kazi wake sambamba Na pongezi kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa
weledi Na ufanisi wa kuwahudumia watanzania Na kauli mbiu ya HapaKaziTu.
No comments:
Post a Comment