Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha jana jioni
ambapo hapo leo ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya
jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva
Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali
jana tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani
Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda
kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani
mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia
korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.
Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili
asubuhi hapo kesho.
Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake
wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na
Viongozi wa wengine wa mkoa huo.
No comments:
Post a Comment