Rais
mstaafu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi(TUCTA) Bi.Magreth Sitta
ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kwa sasa watumishi wamekuwa
wakikumbwa na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya waajiri kutovitambua
vyama hivyo.
Ameyasema
hayo jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi Duniani ambapo kwa upande wa kitaifa maadhimisho hayo
yamefanyikia mkoani Kilimanjaro.
Bi.
Magreth Sitta amesema kuwa, itakuwa ni jambo jema zaidi iwapo kama
waajiri watakaa na wafanyakazi wao na kuziangalia changamoto zilizopo
ili hata Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akizipata aweze kulifikisha suala hilo kwa Spika wa bunge
liweze kutizamwa kwa makini ili kupunguza changamoto husika.
Aliendelea
kusema, serikali na makampuni binafsi hulipa kwa mwezi mishahara duni
ambapo ni ujira mdogo sana kwa siku ikilinganishwa kupanda kwa gharama
za maisha.
Amesema
kwa sasa ukubwa wa kodi ya mapato kwa wafanyakazi (PAYE) kodi ya mapato
inayotozwa na serikali inawalazimisha watumishi wa serikali na sekta
binafsi kulipa kodi mara tatu kwa na zaidi.
Miongoni
mwa ulipaji wa kodi hizo ni pamoja na ulipaji kupitia mishahara yao ya
kila mwezi, kulipa kodi kila wanunuapo bidhaa mbalimbali na ulipaji wa
kodi wakati wa kustaafu.
Aliendelea
kusema kuwa, tatizo lingine kubwa ni baadhi ya taasisi za umma na za
binafsi ambazo zimekuwa zikikwepa kutekeleza sheria za kazi ikiwemo
sheria ya ajira na mahusiano kazini sheria Na. 6 ya mwaka 2004.
Amesema
sheria hiyo inalenga kuwashirikisha wafanyakazi kupitia mabaraza ya
wafanyakazi kupitisha bajeti za taasisi za umma zilizopokelewa Bungeni
bila kuzingatia sheria hiyo hali ambayo imepelekea hali kuwa mbaya zaidi
kwenye makampuni ya tasisi binafsi na kuiomba serikali iwe mfano mzuri
katika kulipa michango ya wafanyakazi katika mifuko iliyopo.
Rais
Mstaafu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi ambaye pia ni mgeni
rasmi B. Magreth Sitta akizungumza na wafanyakazi wa umma na taasisi
binafsi wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika katika
uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
Wanachi
wakimsikiliza Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta leo katika uwanja wa Uhuru
leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya
Jamii.
Rais
Mstaafu Bi. Magreth Sitta akikabidhi cheti cha ushiriki kwa Meneja
Rasilimali watu wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA),Pius Matagi kwa
nimbi ya Mkurugenzi Mkuu leo katika uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es
Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Watumishi
wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) wakishangilia baada ya mtumishi
mwenzao kukabidhiwa cheti cha ushiriki kwa niamba ya Mkurungenzi Mkuu wa
shirika hilo kutoka kwa Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta.
Rais Mstaafu Bi. Magreth Sitta akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbalimbali leo jijini leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wasamalia wema wakiwapatia huduma ya kwanza majeruhi marabaada ya
kuangukiwa na geti katika uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD
marabaada ya kuangukiwa na geti katika uwanja wa Uhuru leo jijini Dar
es Salaam.
Majeruhi akiwa kwenye gari la MSD akiendelea kupewa hudum ya kwanza
No comments:
Post a Comment