Pages

April 8, 2017

Wizara yaipongeza Muhimbili kwa kuandaa Mafunzo Hospitali Binafsi na Umma


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeze Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuendesha warsha ya siku tatu kuhusu upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic surgery) kwa madaktari kutoka hospitali mbalimbali nchini.
Warsha hiyo ilianza jumatano na imemalizika leo Ijumaa na kuwashirikisha madaktari kutoka hospitali ya za jijini Dar es Salaam zikiwamo Kairuki, Tumaini, Regency na Agha kan. Madaktari wengine ni kutoka hospitali za umma zikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana pamoja na hospitali za mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Morogoo na Dodoma.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara hiyo Dk. Dorothy Gwajima kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara, Dk. Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha hiyo.
Dk  Gwajima amewataka washiriki wa warsha hiyo kupeleka ujuzi waliojifunza kwa madaktari wengine ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wanakwenda kutibiwa katika hospitali ya Muhimbili.
“Kwa niaba ya wizara napenda kuipongeza Muhimbili kwa kuandaa mafunzo haya, sisi wizara tunawaunga mkono na msifikiri tumewasahau la hapana kwani tunatambua uwezo wa madaktari. Heshima ya hospitali itabaki pale pale kwani Muhimbili kitovu cha uwanzishwaji wa HospitaOceac road, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Mifupa ya Moi,” amesema Dk Gwajima.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amewashukuru madaktari kutoka hospitali za binafsi na umma kwa kushiriki kwenye mafunzo hayo.
“Tumeanzisha mafunzo haya na napenda kuwahakikishia tutaendelea kuandaa warsha kwa kada nyingine ili kuwajengea uwezo madaktari wa hospitali za mikoa na wilaya nchini,”amesema Profesa Museru.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar ameishauri uongozi wa Muhimbili kuendelea kutoa mafunzo hayo na kuendesha ufapasuaji wa njia ya matundu madogo kwa wagonjwa waliopo mikoani kwani wengi wao hawana fursa ya kupatiwa huduma hiyo.
Washiriki walikabidhiwa vyeti baada ya mafunzo hayo kufungwa.
Katika hatua nyingine, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kutumia njia ya matundu madogo wanaendelea vizuri na baada ya afya zao kurejea katika hali ya kawaida wataruhusiwa kurejea nyumbani.
Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji hadi leo wamefikia wanane.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima akifunga warsha ya siku tatu iliyolenga kuwajengea uwezo madaktari nchini kuhusu upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic Surgery).
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Dk Gwajima wakati wa kufunga mafunzo hayo leo ambayo yamefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Profesa Rafique Parkar akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya upasuaji wa matundu madogo, Dk. Ibrahim Mkoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profea Lawrence Museru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimkabidhi cheti cha ushiriki Dk. Paul Kisanga wa Hospitali ya Selian mkoani Arusha leo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto katika hospitali ya Muhimbili, Zaitun Bhokary akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Profesa Museru.
Daktari bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar (kushoto) akimfanyia upasuaji mmoja wa kinamama mwenye matatizo ya uzazi leo. Kulia ni Dk. Vicenti Tarimo akishirikiana na Profesa Parkar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia upasuaji mubashara katika ukumbi wa mikutano, Muhimbili leo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...