Pages

April 15, 2017

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA TAIFA LA ISRAEL ATEMBELEA SERENGETI NA NGORONGORO

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani wa taifa la Israel,Ehud Barak walipokutana katika eneo la Olduvai Gorge katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro akiwa njiani kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (katikati) ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete.
Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa la Israel,Ehud Barak (kushoto) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani baada ya kukutana katika eneo la Makumbusho ya kale la Olduvai Gorge ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro akiwa njiani kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (kushoto) ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
Mhandisi Ramo Makani akimueleza jambo Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa la Israel ,Ehud Barak baada ya kukutana katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro akiwa njiani kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani (katikati) akimongoza Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa la Israel ,Ehud Barak (kushoto) kutembelea eneo la Olduvai Gorge .kulia ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete.
Waziri Mkuu wa zamani wa taifa la Israel ,Ehud Barak akitia saini katika kitabu cha wageni huku Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akishuhudia mara baada ya kufika eneo la Olduvai Gorge akiwa njiani kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushudia tendo la wanyama aina ya Nyumbu wahamao kwa makundi.
Mhandisi Ramo Makani akimueleza jambo Ehud Barak.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akieleza mambo ambayo amepata kuongea na Waziri Mkuu wa Israel baada ya kukutana nae katika ene la Olduvai Gorge.
Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwa katika picha ya pamoja na Watalii wa ndani baada ya kukutana nao katika eneo la Olduvai Gorge.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...