Mkuu
wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga (kulia) akimpokea Waziri Mkuu
Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alipowasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya
Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017.
Mheshimiwa
Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar (mwenye miwani) akiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya
Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
leo Mkoani Katavi.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na
wananchi (hawapo pichani) waliofika katika viwanja vya Kumbukumbu ya
Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
Waziri
wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akitoa salamu toka Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo
Mkoani Katavi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na
Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo ya mwenge wa uhuru 2017 kwa
mgeni rasmi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani
Katavi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi
Seif Ali Iddi akitoa salamu za Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa
Mkoa wa Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani
Katavi
Watoto
wa alaiki wakitengeneza umbo la mlima Kilimanjaro na kuweka alama ya
mwenge wa uhuru kuashiria kupandisha kwa mwenge huo katika mlima
Kilimanjaro wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani
Katavi.
Wakimbiza
Mwenge Kitaifa wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa
Uhuru kwa ajili ya kukabidhiwa mwenge huo kuukimbiza kwa siku 195 katika
mikoa 31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya
Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi
Seif Ali Iddi akimpa mkono wa baraka kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour kabla ya kumkabidhi mwenge huo
kuukimbiza katika mikoa 31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa
sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja
vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
:
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa
Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto) akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa
sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika
viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi. Watatu
kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour (kushoto)
akimhaidi mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (kulia) kuulinda na kuukimbiza
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote 195 Tanzania bara na Zanzibari
wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017
katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga Mwenge wa
Uhuru baada ya kukabidhiwa mwenge huo na Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi
kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri 195 Tanzania bara na Zanzibar
wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017
katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Watumbuizaji
kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari wakitoa burudani wakati wa
sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja
vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.Picha na: Genofeva
Matemu – WHUSM, Katavi.
Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi
Wananchi
Mkoa wa Katavi wameombwa kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano,
inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika
kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025
na kujenga uchumi wa viwanda nchini.
Rai
hiyo imetolewa na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwenge wa
Uhuru Mkoani Katavi na kusema kuwa Uchumi wa viwanda uliodhamiriwa ni
ule utakaolifanya taifa kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani wa soko
la kimataifa badala ya kuwa chanzo cha malighafi na soko la bidhaa za
viwanda vya mataifa mengine.
“Tanzania
tumeazimia kutoka katika kundi la uchumi duni na kwenda kwenye ujenzi
wa uchumi wa viwanda, Ujenzi na uimarisha wa viwanda nchini ambao
utahusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo, wananchi wenyewe, sekta
binafsi na Mashirika Mbalimbali ya Kimataifa yanayo nafasi kubwa hususan
katika uwekezaji mkubwa, ukuzaji wa mitaji, masoko, Teknologia na
upatikanaji wa rasimali watu wenye ujuzi maalum” amesema Mhe. Balozi
Iddi.
Aidha
Mhe. Balozi Iddi amesema kuwa wananchi wanayo fursa kubwa sana katika
kujenga na kuendeleza viwanda nchini kwani ukuaji wa uchumi wa Viwanda
unaanza kwa jitihada za wananchi wenyewe katika kuanzisha na kuendesha
viwanda vidogo vidogo vinavyoweza kuongeza thamani ya mazao na bidhaa
wanazozalisha kila siku katika maeneo yanayowazunguka.
Akizungumza
na wananchi wa Mkoa wa Katavi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema
kuwa mbio za mwenge wa uhuru zimekua zikihamasisha amani, mshikamano,
kujenga uzalendo na umoja wa kitaifa kwa kuhamasisha miradi mbalimbali
ya kimaendeleo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ipo sambamba na malengo ya
serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda
kwa kufufua viwanda vilivyopo kuanzisha viwanda vidogo vidogo, viwanda
vya kati na viwanda vikubwa.
Mwaka
huu, ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unahusu Mkakati wa kukuza
Viwanda nchini, chini ya Kauli Mbiu isemayo:- “Shiriki Kukuza Uchumi wa
Viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu”. Ujumbe huu utaambatana na msisitizo
wa Serikali kuhusu mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za
Kulevya na Rushwa.
Mwenge
wa Uhuru uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la
Tanganyika. Hatua hiyo ilikuwa ni utekelezaji wa ndoto yake
iliyotafsiriwa kwa maneno aliyoyatamka mwaka 1958 kwa wajumbe wa Baraza
la kikoloni la kutunga Sheria na kuyarudia tena mwaka 1959 alipohutubia
kikao cha 35 cha Baraza la Umoja wa Mataifa wakati huo akidai Serikali
ya madaraka kama Mbunge mwakilishi pekee wa Tanganyika kwa kusema “Sisi
watu wa Tanganyika, tungependa kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima
Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale
ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipo
jaa dharau”.Falsafa hiyo ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ujumbe
mkubwa kwa Waingereza kwamba, watu wa Tanganyika wamechoka kutawaliwa.
No comments:
Post a Comment