Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu ametembelea
na kukagua kivuko cha MV PANGANI II ambacho kinafanyiwa ukarabati na Kampuni ya
Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza katika eneo la Pangani. Awali kivuko hicho kilikuwa
kikitoa huduma kati ya Pangani na Bweni kabla ya ujio wa kivuko kipya cha MV TANGA.
Dkt.
Mgwatu amejionea kazi zilizokamilika zikiwa ni pamoja na matengenezo ya milango mipya ya
kupandia abiria na magari na sasa kiko katika hatua za mwisho za ukarabati wake. Aidha, Dkt.
Mgwatu aliweza pia kusafiri kutoka upande wa Pangani hadi Bweni kwa kutumia boti mpya ya
MV BWENI iliyojengwa hivi karibuni kwa ajili ya matumizi ya dharura katika eneo hilo.
Akiwa katika ukaguzi huo, Dkt. Mgwatu aliambatana na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Tanga
Mhandisi Margaret Gina, Mkuu wa Kivuko cha Pangani Bw. Abdulrahman Amier pamoja na
baadhi ya wafanyakazi wa TEMESA mkoani Tanga.
Vile vile, Dkt. Mgwatu alipata wasaa wa
kuzungumza na wafanyakazi wa Kivuko cha MV TANGA ambacho kinaendelea kutoa huduma
katika eneo hilo na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii na weledi na kuhakikisha wanaongeza
mapato. Aliwaomba wafanyakazi hao kuitunza boti ya MV BWENI ambayo itatoa huduma za
dharura hasa wakati wa usiku kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa na pia kutoa usafiri mbadala
pale changamoto mbalimbali zitakapojitokeza.
Nae Mhandisi Gina alimueleza Dkt. Mgwatu kero mbalimbali wanazokumbana nazo kivukoni
hapo ikiwemo kukosekana kwa vyumba vya ofisi kwa ajili ya wafanyakazi na kumuomba
awasaidie kupata eneo kwa ajili ya kujenga ofisi. Dkt. Mgwatu alikuwa katika ziara ya kikazi ya
siku moja mkoani Tanga.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu katikati
akishuka kutoka kwenye chumba cha kuongozea
kivuko cha MV Pangani kilichoko Pangani Tanga alipokuwa akikagua
maendeleo ya ukarabati wa kivuko hicho. Nyuma yake ni Mkuu wa Kivuko
Bw. Abdulrahman Ameir.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu wa pili
kulia akikagua Kivuko cha MV Pangani kilichoko Pangani
Tanga kinachofanyiwa ukarabati na kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard
ya jijini Mwanza wakati wa ziara yake mkoani Tanga.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu aliyesimama
katikati akisisitiza jambo wakati akizungumza na
wafanyakazi wa Kivuko cha MV Tanga kinachoendelea kutoa huduma kati ya
Pangani na Bweni mkoani Tanga.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akifurahia jambo na mmoja wa wafanyakazi wa boti ya MV
Bweni mara baada ya kumaliza kikao na wafanyakazi wa TEMESA kituo cha Pangani mkoani Tanga.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu wa tatu kushoto akiwa ndani ya boti ya MV Bweni mara baada
ya kumaliza kukagua kivuko cha MV Pangani kilichoko Pangani mkoani Tanga. Boti hiyo itatoa huduma za dharura ikiwemo kusafirisha
wagonjwa nyakati za usiku.
Muonekano
wa Kivuko cha MV Pangani kilichoko Pangani mkoani Tanga kinachofanyiwa
ukarabati na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard ya
jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment