Pages

April 4, 2017

SHULE YA SONGAMBELE YA MJI MDOGO WA MIRERANI KUJENGEWE MADARASA SABA


Kampuni ya TanzaniteOne kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. 

Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Faisal Juma Shabhai ameahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele ya mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambayo yameweka ufa. 

Tangu mwaka 2013 madarasa hayo yaliweka ufa kutokana na kupitiwa na
mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwenye eneo hilo. 

Kutokana na hali hiyo uongozi wa shule hiyo uliamua kuyafunga madarasa hayo na ofisi ya walimu, wakihofia kupaata madhara kutokana na hitilafu hiyo iliyotokana na tatizo hilo. 

Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Shabhai alisema yeye binafsi atajenga madarasa matatu na wakurugenzi wenzake wa kampuni hiyo Hussein Gonga na Riziwani nao watajenga mengine manne yaliyobakia. 

Alisema kampuni hiyo imeamua kujenga madarasa hayo ili kusaidia jamii inayozunguka maeneo hayo ambayo wao wamewekeza kwenye madini ya Tanzanite. 

“Pamoja na hayo jamii ya eneo hili nanyi mnapaswa kutuunga mkono kwa kutumia nguvu zenu ikiwemo kubeba majabali, matofali na kusogeza mchanga ili tushiriki pamoja,” alisema Shabhai. 

Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Simanjiro Jackson Leskar Sipitieck aliipongeza kampuni ya TanzaniteOne kwa kufikia uamuzi huo kwani utasaidia watoto wa eneo hilo kupata elimu. 

“Mwezi huu kutakuwa na baraza la madiwani na kupitia nafasi hiyo tutatoa shukurani zetu rasmi kwa kutuunga mkono baada ya kujenga madarasa hayo saba ya shule hiii ya Songambele,” alisema Sipitieck.
Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Faisal Shabhai akizungumza kwenye viwanja vya shule ya msingi Songambele Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, alipoahidi wananchi kuwajengea
vyumba saba vya madarasa. 
Mkazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Japhary Matimbwa akiushukuru uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne baada ya kuahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Jackson Sipitieck akiushukuru uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne baada ya kuahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...