Naibu
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Seleman Jafo akiongea na wageni waalikwa
wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa
hafla ya utoa wa matokeo wa Tafiti za Uwezo ambapo alipongeza tafiti za
TWAWEZA na kuwataka watendaji serikalini kuzitumia tafiti hizo ili
kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya elimu, leo Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TWAWEZA Bw. Aidan Eyakuze akiongea na wageni waalikwa
wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa
hafla ya utoa wa matokeo wa Tafiti za Uwezo ambapo aliwaeleza kuwa
Tafiti hii inasaidia kuonesha hali halisi ya iliyopo mashuleni ili
kuboresha sekta ya elimu, leo Mjini Dodoma
Meneja
Uwezo Tanzania Zaida Mgalla akiongea na wageni waalikwa wakiwamo
wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa hafla ya
utoa wa matokeo wa Tafiti za Uwezo ambapo mbali na changamoto nyingine
takwimu mpya za uwezo zinaonesha mwenendo mzuri katika somo la Kiswahili
na uwiano mzuri uliopo kati ya wanafunzi na vitabu, leo Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Seleman Jafo na Mkurugenzi Mtendaji wa
TWAWEZA Bw. Aidan Eyakuze wakimsikiliza Meneja Uwezo Tanzania Zaida
Mgalla wakati akitoa Matokeo ya tafiti za Uwezo Tanzania, leo Mjini
Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TWAWEZA Bw. Aidan Eyakuze akimkabidhi Naibu Waziri Ofisi ya
Rais-TAMISEMI Seleman Jafo matokeo ya Tafiti ya Uwezo Tanzania yaliyopo
katika ripoti ya Je, Watoto wetu wanajifunza? leo Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Seleman Jafo akimkabidhi Mwenyekiti wa
Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba matokeo ya Tafiti ya
Uwezo Tanzania yaliyopo katika ripoti ya Je, Watoto wetu wanajifunza?
leo Mjini Dodoma.
Baadhi
ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakichangia
mjadala mara baada ya kuwasilishwa kwa matokeo ya Tafiti ya Uwezo
Tanzania yaliyopo katika ripoti ya Je, Watoto wetu wanajifunza? Ambapo
walitoa mapendekezo kwa Serikali yenye lengo la kuboresha sekta ya elimu
Nchini. PICHA NA HASSAN SILAYO
Serikali imewataka watendaji serikalini kuzifanyia kazi tafiti mbalimbali zinazotolewa na asasi za kiraia ili kuleta matokeo chanya na kuboresha maisha ya watanzania.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo wakati akipokea ripoti ya Takwimu Mpya za Uwezo Tanzania iliyopo katika TWAWEZA.
Akiongea katika Hafla hiyo Naibu Waziri Jafo amesema kuwa Watendaji Serikalini sasa wana budi wa kufanyia kazi tafiti mbalimbali zinazotolewa na Azaki za kiraia zinazolenga masuala yaliyopo katika jamii ili kuiwezesha serikali kuyafanyia kazi matokeo ya tafiti na kuboresha hali ya watanzania.
“Kwa matokeo haya ya Tafiti ya TWAWEZA kupitia Uwezo Tanzania ni kipimo tosha cha kutuonesha sisi kama viongozi yapi tunayotakiwa kufanya na yapi hatutakiwi kufanya na yapi tunatakiwa tuyarekekebishe katika sekta ya elimu na matokeo haya tutayafanyia kazi”-Naibu Waziri Jafo.
Aidha Naibu Waziri Jafo aliwastaka wabunge kutumia vikao muhimu vya kisheria kwenye maeneo yao ya kazi katika kuhakikisha matokeo ya tafiti yanasaidia kuboresha sekta ya elimu katika Halmashauri huku serikali ikiendelea kuwekeza katika sekta ya elimu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze alisema kuwa tathmini hii inayopima matokeo ya kujifunza ambayo ambayo ni kubwa barani afrika inayotekelezwa kwenye baadhi ya nchi ikiwamo Kameruni, Nigeria, Senegali,Mali, Ghana na Burkina Faso inasaidia kuonesha hali halisi ya iliyopo mashuleni ili kuboresha sekta ya elimu.
Naye Meneja wa Uwezo Tanzania Zaida Mgalla amewataka viongozi wa Serikali na wabunge kutumia tafiti hii ya uwezo katika kuhakikisha wanashiriki katika kuboresha elimu katika maeneo yao na Tanzania kwa Ujumla ikiwa ni lengo kuu la kuhahakikisha wanaifikisha sekta ya elimu pale inapotakiwa.
No comments:
Post a Comment