Othman Khamis Ame, OMPR
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitiza kauli yake inayotoa kila mara ya
kuwataka Wananchi wanaoishi Mabondeni na sehemu nyengine hatarishi zenye
kujaa maji wakati wa msimu wa mvua za Masika kuhama mapema ili
kujiepusha na athari zinazoweza kuleta maafa.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi wakati akiwapa pole wananchi wa Kazole Kwagube ambao nyumba zao
zipatazo 37 zimeathirika kutokana na upepo mkali uliovuma Jumapili
iliyopita ambapo kati ya hizo Nyumba 22 zinahitaji matengenezo.
Balozi
Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikitoa matangazo
kuhusiana na maeneo hayo hatarishi na haitakuwa tayari kuwa na mpango
wa kuweka Kambi kama inavyofanya katika miaka ya nyuma kwa ajili ya
kuwahifadhi kwa muda watu wanaoishi mabondeni watakaoathirika na mvua za
masika.
Alisema
inasikitisha kuona kwamba wapo baadhi ya Watu wanaendelea na tabia ya
kukaidi maagizo yanayotolewa na Serikali na matokeo yake hutoa kauli
zisiazostahiki licha ya kwamba wao ndio walalamikaji wakubwa wakati
wanapokumbwa na kadhia kama hizo.
Akiwapa
pole Wananchi hao wa Kwagube ambao wamo ndani ya Majimbo ya Kiwengwa na
Mahonda Balozi Seif alisema maafa hayategemewi kama muathirika anaweza
kupata muda wa kujitayarisha katika kukabiliana nayo.
Alitahadharisha
kwamba hali ya Hewa hivi sasa imebadilika kiasi kwamba Wananchi
Wanapojitayarisha kujenga Nyumba za makaazi wazingatie ujenzi unaoweza
kukabili mazingira yoyote yanayotokezea.
Balozi
Seif aliwaasa Wananchi kwamba mpango wa kujenga nyumba na kuezeka mapaa
kwa kutumia njia ya kulaza mabati kwa kidhibiti cha matofali au mawe
waelewe kuwa njia hiyo inaweza kuleta athari kubwa hasa wakati
unapotokea upepo mkali katika maeneo yao.
Mapema
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd.
Ali Juma Hamad alisema Wataalamu wa Kamisheni yake tayari wameshafanya
Tathmini ya athari ya upepo huo ingawa Serikali haitakuwa na nguvu kubwa
za kusaidia kurejesha hali ya kawaida kwa Nyumba zilizoharibika na
upepo huo.
Nd.
Juma alisema tathmini hiyo imetoa muelekeo na kubainisha gharama
zilizojichomoza ndani ya zoezi hilo zinazokadiriwa kufikia kati ya
shilingi Laki Moja hadi saba kwa nyumba zipatazo 22 kati ya zile 27
zilizoathirika na upepo huo.
Katika
Mkutano huo wa kuwapa pole waathirika wa upepo huo Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikabidhi Fedha kwa Familia za waathirika
22 kati ya 27 kulingana na tathmini iliyopigwa ya kila nyumba ili
zisaidie nguvu za familia hizo kurejesha hali yao ya kawaida.
Waathirika
hao ni Bibi Asha Salum, Bwana Makame Juma, Bwana Bakari Daudi, Nd.
Ayoub Makame, Bibi Afua Faki, Nd. Suleiman Abdulla, Nd. Haji Zubeir, Nd.
Silima Jongo na Nd. Ali Khamis.
Wengine
ni Hassan Mohamed, Nd. Khamis Haji, Nd. Abdalla Ibrahim, Bwana Makame
aliyetambulika kwa jina moja tu, Nd. Khamis Bakari, Nd. Hija Abdulla,
Nd. Makame Wadi, Nd. Khamis Khamis, Nd. Mngwali Khamis, Nd. Zawadi
Suleiman, Nd. Ussi Khamis, Nd. Yahya Aman na Nd. Khalfan Khamis Hilal.
No comments:
Post a Comment