Pages

April 14, 2017

ASKARI POLISI NANE WAUAWA KWA KUFYATULIWA RISASI MKOANI PWANI

Ikwiriri. Polisi saba waliokuwa doria katika Kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, wanadaiwa kuuawa usiku wa kumkia leo kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, lakini akasema taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani.

Taarifa za uhakika zilizolifikia Mwananchi Digital zimeeleza kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewasili eneo yalipotokea mauaji ya askari wanane katika kijiji cha Jaribu, Wilayani Kibiti leo.

Waziri Nchemba ameambatana na naibu wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni. Nchemba atatembelea kambi za askari polisi wa kanda ya Pwani na katika kata ya Bungu wilayani Kibiti.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...