WANAWAKE WATAKA WAPEWE NAFASI ZA MAAMUZI

Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika(EAC)wakipita kwa matembezi kwenye mitaa ya jiji la Arusha katika maadhimisho ya Siku ya wanawake kimataifa yaliyofanyika jana.Picha na Filbert Rweyemamu

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ),Monduli mkoa wa Arusha wakiongoza matembezi ya maadhimisho ya siku ya Wanawake kimataifa yaliyofanyika makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)

Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika(EAC)wakipita kwa matembezi kwenye mitaa ya jiji la Arusha katika maadhimisho ya Siku ya wanawake.


Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika(EAC) na wananchi wakipita kwa matembezi kwenye mitaa ya jiji la Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika(EAC),Utawala na Fedha,Jesca Eriyo akizungumza katika eneo la Soko Kuu jijini Arusha.

Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Ruth Simba akishiriki kufanya usafi kwenye Soko Kuu la Jiji la Arusha

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika(EAC),Utawala na Fedha,Jesca Eriyo aliyeinua mkono juu zaidi akizungumza katika eneo la Soko Kuu jijini Arusha.        


Filbert Rweyemamu
Arusha.Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) anayeshughulikia Utawala na Fedha,Jesca Eriyo amekosoa mfumo dume unaozuia idadi kubwa ya wanawake kuwa katika nafasi za maamuzi.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika katika Soko Kuu la jiji la Arusha alisema haoni sababu za wanawake kuendelea kufanyakazi za chini wakati wanaweza kufanya kazi zote za kitaalamu.

"Mfumo dume umetawala sana na mgumu kuuvunja hasa kwetu waafrika,katika Jumuiya ya Afrika Mashariki niko mwanamke pekee kati ya wanaume sita kwenye ngazi ya juu ya menejimenti,vilevile hata ngazi ya Wakurugenzi yupo mwanamke mmoja huku wanaume wapo saba,"alisema Eriyo

Maadhimisho yao yaliandaliwa na wanawake wanaofanya kazi jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na asasi za wanawake na vijana zinazohusika na harakati za kuyajengea uwezo makundi hayo.

Naibu Katibu Mkuu huyo aliwaongoza wanawake kufanya usafi na kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi kwa jiji la Arusha ili kusaidia juhudi za kuuweka mji huo katika hali ya usafi wakati wote.

"Tumetoa vifaa hivi hasa vya usalama ili kuwawezesha wanawake ambao wengi wao ndio wanaofanya kazi za usafi wawe salama kiafya ili kuendelea kusaidia familia zao,"alisema Eriyo

Naye Mratibu wa taasisi ya Widows Empowerment and HIV/AIDS Foundation(WEHAF),Halima Mohamed alisema maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ina maana kubwa kwani inawaleta pamoja wanawake kujadili changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.

"Wanawake wengi wameachiwa majukumu ya kutunza familia na ukizingatia mfumo dume uliwanyima elimu kwahiyo wanafanya kazi ngumu na zenye malipo duni sana,"alisema

Kwa upande Afisa Mipango Miji wa Jiji la Arusha,Mariam Kimolo alisema wanawake wana mchango mkubwa katika ustawi wa familia na taifa kwa ujumla na serikali inatambua mchango kwa kuwapa nafasi za uongozi.



Post a Comment

أحدث أقدم