Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt.Ashatu Kijaji, ameipongeza kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC kuwa ya kwanza kutekeleza sheria ya
EPOCA na sheria ya fedha ya mwaka 2016 kwa kuuza hisa zake kwa Umma
kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na alitoa rai kwa
watanzania,makampuni ya kitanzania na taasisi za serikali kujitokeza
kununua hisa hizo baada ya kusoma waraka wa matarajio wenye mwongozo wa
ununuaji wa hisa za kampuni hiyo.
Akiongea
wakati wa Uzinduzi wa uuzaji wa hisa za kampuni hiyo uliofanyika
jijini Dar e salaam, Dkt.Kijaji alisema kuwa uwekezaji huu utakuza
shughuli za soko kwa asilimia kubwa “Hivi sasa wawekezaji katika hisa
kwenye masoko ya mitaji hapa nchini ni takribani laki tano,hivyo iwapo
wateja wote wa Vodacom milioni 12.4 watashiriki katika ununuzi wa hisa
utaongeza uwekezaji wa hisa kupitia masoko ya mitaji katika soko la
hisa kwa asilimia 2,380%.
Alisema
haya yatakuwa ni mageuzi makubwa katika sekta ya masoko ya mitaji na
fedha si hapa nchini tu bali hata katika ukanda wa Afrika Mashariki
kwani hivi sasa Kenya ina wawekezaji wapatao 1,700,000,Uganda 40,000 na
Rwanda 14,000.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao
amesema, “Tunayo furaha kuifikia siku ya leo ambapo tumefungua milango
kwa wananchi wa Tanzania na tunawakaribisha wanaotaka kuwekeza katika
safari hii ambayo tumeianza.Tukio hili ni la kihistoria katika sekta ya
mawasiliano nchini Tanzania, Vodacom Tanzania imekuwa kampuni ya kwanza
ya mawasiliano hapa nchini kuandika historia ya kuuza hisa zake kwa umma
kupitia Soko la benki ya NBC yenye matawi nchi nzima na mawakala kwa
kuuza hisa kuwashirikisha watanzania wote katika safari ya mafanikio ya
kampuni yetu”.
Ferrao
alisema kuwa kuanzia leo,asilimia 25% za kampuni ya Vodacom Tanzania
PLC zitauzwa kwa watanzania kutokana na kibali kutoka serikalini kupitia
Mamlaka ya Dhamana Masoko na mitaji (CMSA)-“Kutokana na matakwa ya
sheria hadi kufikia hatua hii tumepata ushirikiano mkubwa kutoka taasisi
za serikali za CMSA ,DSE na wadau wengine,nashukuru kwa ushirikiano huu
ambao umefanikisha mchakato mzima na leo wateja wetu nchini kote na
taasisi mbalimbali za kitanzania zinazo fursa ya wabia wetu kupitia
ununuaji huu wa hisa”Aliongeza.
Kuhusiana
na mchakato mzima wa ununuaji wa hisa alisema “Kutokana na kuzinduliwa
mchakato wa uuzaji hisa kuanzia leo,wanaohitaji kununua hisa watazipata
kwa kutembelea matawi yote ya Benki ya NBC na mawakala wa Soko la Hisa
la Dar es Salaam (DSE) waliopo nchi nzima “.Alitoa msisitizo kuwa kila
hisa itauzwa kwa shilingi 850/-na asilimia 25% ya hisa zinazotarajiwa
kuuzwa zina thamani ya shilingi Bilioni 476.
Ferrao
alimalizia kwa kusema “Vodacom Tanzania PLC inayo dhamira ya kweli ya
kuendelea kuwekeza nchini na kukuza sekta ya mawasiliano na kufanikisha
malengo yake makuu ambayo ni kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa
kidigitali,kuwaunganisha watanzania katika mtandao wake na kubadilisha
maisha ya wananchi kuwa murua kupitia ubunifu mkubwa wa kiteknolojia.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao(kushoto)akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa(hawapo pichani)wakati wa
Uzinduzi wa Uuzaji wa hisa za kampuni hiyo kwa Umma leo jijini Dar es
Salaam,Waliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za kibenki
kwa makampuni wa NBC,Theobald Sabi, Mkuu wa kitengo cha huduma za
Uwekezaji wa hisa za makampuni wa Orbit Securities,Godfrey Gabriel na
Mkurugenzi wa fedha wa Vodacom Tanzania PLC, Jacques Marais.
Naibu
Waziri wa fedha na Mipango,Dkt.Ashuta Kijaji(watatu kushoto) Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao(kushoto kwake)Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Usimazi wa Mawasiliano(TCRA) Eng.James
Kilaba(kushoto)Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania PLC,Vivek
Mathur(wanne kushoto)na Mkurugerugenzi wa kitengo cha biashara za
Vodacom Tanzania PLC,Gregory Verbond,wakiponyeza kitufe kuashiria
Uzinduzi wa Uuzaji wa hisa za Vodacom Tanzania PLC kwa Umma leo jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa fedha na Mipango,Dkt.Ashuta Kijaji(katikati)akiagana na
Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania PLC,Vivek Mathur(kulia)baada ya
kuzindua Uuzaji wa hisa za Vodacom Tanzania PLC kwa Umma leo jijini Dar
es Salaam,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao.
Naibu
Waziri wa fedha na Mipango,Dkt.Ashatu Kijaji(kushoto)akimsikiliza jambo
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao,baada ya
kuzindua rasmi Uuzaji wa hisa za Vodacom Tanzania PLC kwa Umma leo
jijini Dar es Salaam.
Kutoka
kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao,Mkuu wa
kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni wa NBC,Theobald
Sabi,Mkurugenzi wa fedha wa Vodacom Tanzania PLC, Jacques
Marais,Wakimsiki Mkuu wa kitengo cha huduma za Uwekezaji wa hisa za
makampuni wa Orbit Securities,Godfrey Gabriel(katikati)alipokuwa akijibu
swali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa
Uuzaji wa hisa za kampuni hiyo kwa Umma leo jijini Dar es Salaam.







Post a Comment