Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Ilobi kata ya Mwaweja alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Katibu
Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kishapu, Stephen Magoiga akitoa neno la shukurani kwa mkuu wa mkoa.
Wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wakifuatilia mkutano wa hadhara
kijiji cha Ilobi kata ya Mwaweja wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa
wilayani humo
Mmoja
wa wananchi wa kijiji cha Ilobi akitoa kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Zainab Telack wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo.
Wananchi wa kijiji cha Ilobi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wakati akizungumza nao kuhusu maendeleo alipofanya ziara ya kikazi.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ametoa msaada wa mabati 171 kwa
shule za msingi tatu wilayani Kishapu mkoani hapa kwa ajili ya kuezekea
vyumba vya madarasa pindi yatakapokamilika ujenzi wake.
Telack
alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Ilobi, kata ya Mwaweja wilayani hapa alipofanya ziara ya kikazi ambapo
pia alitumia nafasi hiyo kusikiliza kero zao.
Katika
msaada huo jumla ya shule tatu za Nyenze iliyopo kata ya Idukilo,
Mwasubi kata ya Bunambiyu na Ilobi kwenye kata ya Mwaweja zitanufaika na
msaada huo wa mabati 57 kila moja.
Akiwa
katika ziara hiyo ya kikazi wilayani hapa, Telack aliagiza wazazi wote
kijijini hapo wawapeleke watoto wao na kuwaandikisha shuleni ambapo
alisisitiza umuhimu wa elimu kwao.
Mkuu
huyo wa mkoa alitoa onyo kwa wazazi ambao watashindwa kuwapeleka watoto
wao shuleni watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe
fundisho kwa wengine.
Alizungumzia
umuhimu wa elimu kuwa ni haki ya kila mtoto hivyo wazazi ni wajibu wao
kuhakikisha wanawaandikisha shule badala ya kuwaachia mzigo wa kufanya
shughuli za shambani au kuwaozesha.
”Watoto
siyo mali wala ng’ombe bali ni wenzetu na ni wakombozi tunataka wakuu
wa mikoa watoke hapa, tunataka hata rais atoke hapa kijijini hivyo
naagiza kila mtoto aende shule, kamateni wazazi ambao watoto wao hawapo
shule,” alisema.
Aidha,
Telack aliwahimiza wananchi kijijini hapo na wilaya kwa ujumla kutumia
fursa ya kulima mazao ya biashara yakiwemo alizeti, na pamba ili
wajipatie kipato na kuendesha maisha yao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kishapu, Stephen
Magoiga alimshukuru mkuu wa mkoa kwa msaada huo wa mabati na kuahidi
kuchangia saruji na mbao za kumalizia kuezekea vyumba vya madarasa.
Aliwahimiza
wananchi kuendelea na kuchangia shughuli za maendeleo kwa kujenga
vyumba vya madarasa hadi kufikia hatua ya boma ambapo halmashauri
itamalizia ujenzi huo.
Magoiga
alimuahidi mkuu wa mkoa kuwa halmashauri itakamilisha miradi hiyo ya
ujenzi wa madarasa kupitia nguvu za wananchi ambapo alimualika kuizindua
rasmi pindi itakapokamilik

إرسال تعليق