MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH: PAUL MAKONDA AKAZINDUA BARABARA

Katika jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuendeleza na  kubadilisha muonekano wa  jiji la Dar es salaam kufikia viwango vya majiji ya kimataifa leo hii amegusa idara ya miundo mbinu ya barabara ambayo ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile. 
Ombi la ujenzi wa miundo mbinu ya barabara ya bandari via kidongo chekundu yenye urefu wa  km 1 ambayo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari yetu hapa nchini lilitolewa na Mh Mkuu wa Mkoa miezi 2 iliyopita kwa kampuni ya ujenzi ya kizalendo ya Grant Tech Company ya hapa jijin

 Mkandarasi huyo (Grant tech) alikubali na kuanza kazi mara moja kama sehemu ya kuunga mkono utendeji kazi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam.Leo hii mkandarasi huyu amekabidhi barabara iliyokamilika kwa kiwango cha zege yenye zaidi ya thamani ya mil 750.
 Mkuu wa mkoa amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ndoto ya Mh  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda  inaendelea kutimia.
 Katika hgafla hiyo fupi ya makabidhiano RC makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema fedha za barabara ili kupunguza bugudha za usafiri kwa  wananchi wa Dar es salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta haza hata kwa vyombo vyao vya usafiri.Pia Mh Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kali kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa  kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini  kwa miaka mitatu.
 
 
 
Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi 6 haijapita".
Hayo yote yamesemwa leo na Mh Makonda katika uzinduzi huo

Post a Comment

أحدث أقدم