Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa ufafanuzi wa
muongozo wa ukusanyaji wa mapato kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa
Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
MD Kayombo akisisitiza jambo
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Maafisa
Watendaji wa Kata 14, Watendaji wa Mitaa 91 pamoja na Wahasibu wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameonywa kutopokea Rushwa wala hongo
ya aina yoyote kutoka kwa wamiliki wa biashara mbalimbali katika
Manispaa hiyo kwani kufanya hivyo watadhoofisha ukusanyaji wa mapato ya
serikali kama ilivyokusudiwa.
Kauli
ya onyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi
Kayombo wakati akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato na
kutoa maelekezo ya majukumu ya kazi kwa Maafisa Watendaji wa Kata na
Mitaa kwenye kikao cha kazi kilichofanyika leo Jumamosi Machi 18, 2017
katika ukumbi wa Ofisi za Manispaa hiyo ilipo Mtaa wa Kibamba CCM.
Kayombo
ameeleza kuwa kwa mtumishi yoyote wa Manispaa kwa ngazi yoyote
atakayebainika kujihusisha na ubadhilifu kwa kuchukua Rushwa kwa walipa
kodi atachukuliwa hatua Kali za kisheria kwa kuiibia serikali kwani
kuihujumu serikali kwa kuiibia mapato au kuzuia ukusanyaji wa mapato ni
kosa kwa mujibu wa taratibu na sheria.
“Nina
amini kwamba mnaishi vizuri na wananchi wenu kwahiyo mnawafahamu vizuri
wafanyabiashara wanaokwepa kulipa Kodi lakini hata walipaji wazuri hivyo
jambo la ukusanyaji mapato litakuwa jepesi sana kwenu kutokana na
uzoefu mlionao” Aliongeza Kayombo
Mkurugenzi
huyo amewasisitiza Watendaji hao kusimamia vyanzo vyote vya mapato
ikiwemo Hotel Levy, Service Levy, Mabango makubwa na madogo (Bill
Board), Leseni za biashara na Vileo, Upimaji afya kwa ngazi za Mitaa
hususani katika Migahawa.
Hata
hivyo amewataka Watendaji hao kufanya kazi kwa ushirikiano, Uaminifu, na
Weledi mkubwa kwani kufanya hivyo kutasababisha ukusanyaji mkubwa wa
Mapato kwa mwaka 2016/2017.
Kayombo
Amewataka Watendaji wote kukagua Maduka yote katika maeneo yao ya kazi
ili kubaini Maduka yasiyokuwa na leseni na Yale yenye leseni kuwa na
Leseni za Manispaa ya Ubungo kwani wafanyabiashara wa Maduka mengi
wamekuwa na kisingizio cha kukata leseni na Kodi mbalimbali katika
Manispaa ya Kinondoni na kutaka kulazimisha kuitumia leseni hiyo kama
halali kwa Manispaa ya Ubungo.
Sambamba
na hayo pia MD Kayombo amewataka Maafisa biashara kutochelewesha leseni
za wafanyabishara waliokamilisha taratibu zote za kumiliki leseni kwani
kufanya hivyo ni kuchelewesha huduma kwa wananchi na kuongeza makwazo
kwa wafanyabishara kwa sababu tu ya kuchelewa kusaini leseni.
Alisema
kuwa litakuwa ni jambo la aibu na lisilovumiliwa kwa kuruhusu sheria
zitungwe kwa umakini mkubwa lakini utekelezaji wake uwe hafifu.
MD
Kayombo aliongeza kwa kusema kuwa hakuna Haki bila wajibu hivyo
Watendaji hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea lakini pia kutofanya kazi
kwa kuongozwa na tamaa.
MD
Kayombo amesema kuwa Oparesheni hiyo ya itakayodumu kwa miezi mitatu ya
ukusanyaji wa mapato itaanza jumatatu Machi 20, 2017 kwa ushirikiano
baina ya watendaji kutoka Makao makuu ya Wilaya, Watendaji wa Kata,
Watendaji wa Mitaa na wenyeviti wa serikali za Mitaa.






إرسال تعليق