Mgeni
rasmi wa Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango akitoa hotuba yake
wakati akiufungua Mkutano huo, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha. Akifungua Mkutano humo, Waziri Mpango
ameupongeza Mfuko huo kwa kwa kutekeleza kwa vitendo Mpango wa pili wa
Maendeleo ya Taifa wa Miaka mitano na kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa
nchi ya Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2015 kupitia kwenye uwekezaji wa
viwanda. akilizungumzia swala la waajiri wenye tabia ya kutowaunganisha
wafanyakazi wao na mifuko ya jamii, Waziri Mpango amesema kufanya hivyo
ni kwenda kinyume na sheria ya nchi, hivyo amewataka Waajiri wenye tabia
hiyo kuacha mara moja.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni
Rasmi kufungua Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni
wa PPF, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC,
Jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Hijjah akihutubia katika
ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini
Arusha.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akitoa taarifa fupi ya
Mfuko kwa Wadau na Wanachama, katika Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.
Mkurugenzi
wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Martin Mmari akiwasilisha
mada katika Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini
Arusha.

Sehemu
Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifatilia Mkutano huop
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.
Sehemu wa Wakurugenzi wa Mifuko ya Jamii, wakiwa katika Mkutano huo.




























Post a Comment