Waziri
Mkuu Kasim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha kuengeneza nyuzi
za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne
De Textile Ltee kilichopo nje kidogo ya mji wa Port Louis nchini
Mauritious. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nguo zilizoshonwa kwa vitambaa
vilivyotengenezwa na kwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile
Ltee cha Mauritius wakati alipotembelea kiwanda hicho, nje kidogo ya
mji wa Port Louis nchini Mauritius, Machi 22, 2017.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza viongozi wa kiwanda cha nguo cha
Mauritius cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee baada ya kutembelea
kiwanda hicho kilichopo nje kidogo ya mji wa Port Louis Machi 22, 2017.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Compagnie Mauricienne De
Textile Ltee kinachotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa
nchini Mauritius chenye uwezo wa kutengeneza tani milioni 40 hadi 50 kwa
mwaka.
Aidha,
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao kuja
nchini Tanzania na kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi pamoja
na nguo kwa kuwa kuna malighafi za kutosha kwa ajili ya uzalishaji huo.
Waziri
Mkuu alitembelea kiwanda hicho kilichoko katika mji wa Latour Koenig
jana (Jumatano, Machi 22, 2017) na kujionea namna wanavyotengeneza nguo
kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kuamua kuwakaribisha waje kuwekeza
nchini.
“Tumefarijika
na uwekezaji wenu na tumejionea namna ambavyo mnavyoendesha kiwanda
chenu kuanzia utengenezaji wa nyuzi hadi nguo, hivyo tunahitaji viwanda
kama hivi nchini Tanzania kwa sababu sisi tunazalisha pamba nvingi na
yenye ubora unaokubalika kimataifa,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema madhumuni ya kuwakaribisha wawekezaji hao kuja Tanzania
na kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi yanalenga kuboresha
kilimo cha pamba na kuwawezesha wakulima kupata tija.
“Tunalima
pamba nzuri na hawa hawalimi wananunua kutoka nje ya nchi yao, hivyo
wakija kuwekeza Tanzania itawarahisishia kupata malighafi ya uhakika na
kwa urahisi ” alisema.
Alisema
viwanda hivyo vitasaidia maendeleo ya kilimo cha pamba kwa sababu
vitatoa ajira kwa wananchi wengi hivyo kuwawezesha kujikwamua kiuchumi
na kuondokana na umasikini wa kipato.
Mbali
na kuwakaribisha wawekezaji hao, pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa
wananchi wenye uwezo kuhakikisha wanajenga viwanda vya nyuzi kwenye
mikoa yote inayozalisha pamba ili waweze kuiongezea thamani kabla ya
kuiuza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa kiwanda hicho Bw. David Too Sai Voon
alisema wamefurahishwa na mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya
kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya nyuzi na nguo.
Bw.
David alisema kiwanda chao kilianzishwa mwaka 1986 na kwa sasa
kimeajiri wafanyakazi 18,000 ambapo mauzo yao kwa ni dola milioni 200.
“Nguo tunazotengeza ni za kiwango cha kimataifa na tunauza katika maduka
makubwa barani Ulaya,”
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MACHI 23, 2017.
No comments:
Post a Comment