Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao kazi cha Shirika
la Uzalishaji mali la Magereza ambapo katika Kikao hicho cha siku mbili
Wakuu wa miradi watapata fursa ya kuelezea maendeleo ya miradi
mbalimbali ya shirika hilo. Kikao hicho kimeanza leo Machi 15, 2017
katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wakuu wa miradi mbalimbali ya Shirika la Magereza wakifuatilia kwa
makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa katika Kikao kazi cha Shirika la Uzalishaji Mali la
Magereza(hayupo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akimkaribisha Mkurugenzi wa
Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Bw. David Mwangosi ambaye
alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi katika
ufunguzi wa Kikao kazi hicho.
Meza
Kuu ikiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(kulia) akitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali(kushoto) ni Mdhibi
Mkuu wa Shirika la Magereza, ACP. Joel Bukuku(katikati) ni Kamishna wa
Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Mkuu wa Magereza Mkoa Mara, ACP. Goleha Masunzu akichangia hoja katika Kikao hicho.
Mkurugenzi
wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Bw. David Mwangosi
ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi
katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Shirika la Magereza (wa pili toka
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Miradi ya Shirika la
Magereza(wa pili toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa
Magereza, Edith Mallya (Picha zote na Jeshi la Magereza).


إرسال تعليق