Mke
wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel amesema mapinduzi
yanayotakiwa kufanyika hapa nchini kwa sasa ni ya kuwainua wanawake
kiuchumi, kiafya na kijamii.
Mama
Machel, ambaye ni mke wa Hayati Nelson Mandela amesema hayo leo Ijumaa
wakati wa mkutano na wanahabari alipozindua mpango wa kuwainua wanawake
Afrika."Mapinduzi ya kwanza yalifanikiwa wakati ule tunatafuta uhuru
lakini,"amesema.
Mama
Machel amesema wanawake hawana budi kushika usukani katika kuhakikisha
wanafanikiwa kiuchumi na katika sekta zote za maendeleo.
Kwa
upande wake Mwanzilishi wa Tanzania Women Chambers, Anjelina Maleko
amesema kama wanawake wamebarikiwa kwa jambo moja hawana budi kuwa
baraka kwa wenzao.
Mke
wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel akizungumza na
waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kuhusu changamoto
wanazozipata wanawake kiuchumi na katika sekta zote za maendeleo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwainua wanawake Afrika uliofanyika katika leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida
Waziri akiongea akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa Mke
wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini mama Graca Machel alivyomsaidia
kufikia malengo hasa kwenye suala la elimu.
Mwenyekiti
wa chama cha wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Jacqueline
Mneney Maleko akizungumzia mafanikio yake pamoja na njia wanazoweza
kuzitumia wanawake ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Baadhi
ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye
uzinduzi wa mpango wa kuwainua wanawake Afrika na Tanzania ikiwa nchi
ya kwanza.
Mke
wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel(katikati) akiwa kwenye
picha ya pamoja na Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA
Construction Limited Bi. Maida Waziri(kushoto)
Mke
wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel akizungumza na mmoja
waadishi wa habari mara baada ya kufanyika uzinduzi wa uzinduzi wa
mpango wa kuwainua wanawake Afrika.

إرسال تعليق