Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo amesema kuwa fedha
zinazotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa miji
zinatakiwa kusimamiwa kwa umakini.
Jaffo
ameyasema hayo leo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja katika
eneo la Tuangoma jijini Dar es Salaam, amesema kuwa Temeke inakwenda
kwa kasi katika utekelezaji wa mradi uboreshaji wa miji.
Amesema
kuwa baada ya miaka mitano jiji la Dar es Salaam itakuwa imebadilika
kutokana na mradi wa uboreshaji miji na kuondokana na mafuriko ya mara
kwa mara inayotokana na tatizo la miundombinu.
Jaffo
amesema wakandarasi wanaosimamia miradi lazima wafanye kazi kwa
kufatilia ili miradi hii iweze kudumu kwa muda mrefu na sio kuwa miradi
ambayo baada ya mwaka mmoja kukamilika na kuanza nyufa.
Aliongeza
kuwa watu ambao wanatakiwa kufidiwa atafatilia kwa mthamini mkuu wa
serikali waweze kufidiwa ili mradi uende kwa kasi na Temeke iwe ya
kwanza kuwa mji wa kisasa.
Aidha
amesema kwa kutokana na mradi huo uko chini ya ofisi yake atafatilia kwa
ukaribu katika kuhakikisha jiji la Dar es Salaam linakuwa na ubora na
maji mengine duniani.
.Naibu
Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akizungumza na watendaji
wa Manispaa ya Temeke pamoja na wakandarasi wa mradi wa uboreshaji miji
DMDP la Tuangoma leo alipofanya ziara katika maradi huo.picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
.Mkuu
wa Wilaya ya Temeke , Felix Lyaniva akimpa maelezo Naibu Waziri Ofisi ya
Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo juu ya mradi wa Mji wa Temeke katika eneo
la Tuangoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akiwa katika picha ya
pamoja na watendaji wa manispaa ya Temeke na wakandarasi wa mradi DMDP.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akiwa katika picha pamoja
na wakandarasi wa mradi wa DMDP leo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya
Jamii.
Muonekano wa mradi katika mji waTuangoma leo

Post a Comment