Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaagiza watendaji wa serikali
kuanzia ngazi ya kitongoji hadi Mkoa kusimamia na kuwa walinzi wa
kwanza wa miundombinu ya miradi yote inayotekelezwa na serikali pamoja
na wahisani hasa miundombinu ya maji ambayo imekosa usimamizi wa
kutosha.
Dkt.
Nchimbi ametoa agizo hilo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji
mara baada ya kusimamia makabidhiano ya mradi wa maji ulioibuliwa na
halmashauri ya Iramba kabla ya kuundwa kwa halmashauri ya Mkalama ulipo
mradi wa maji wa Iguguno wenye thamani ya shilingi milioni 847,099,550
na unahudumia watu elfu kumi.
Amesisitiza
kuwa serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakitumia fedha nyingi
kutengeneza miradi ya maji ili kuwapunguzia wananchi adha ya upatikanaji
wa maji safi na salama ambapo miradi hiyo imekuwa haileti mafanikio
yaliyotarajiwa kutokana na kukoa usimamizi wa kutosha.
“Naelekeza
taarifa ya miradi yote ya maji iletwe ofisini kwangu, nataka nifahamu
miradi ambayo imefikia lengo la kuwapatia wananachi maji na ile ambayo
wananchi hawajaanza kunufaika kwa kupata maji safi na salama lakini
fedha za umma zimetumika”, amesema Dokta Nchimbi.
Aidha,
Dkt. Nchimbi amewaaigiza watendaji wa vijiji na kata kusimamia na
kutunza miundo mbinu mbalimbali ikiwemo ya maji katika maeneo yao huku
akielekeza kuwa endapo uharibifu utatokea mtendaji aliyepo katika eneo
husika atawajibishwa kwa uzembe.
Awali
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Nchimbi ametembelea chanzo cha maji cha
Mwankoko kinachotoa maji katika halmashauri ya manispaa ya Singida na
kisha kupanda miti ili kutunza mazingira na kuhifadhi chanzo hizo.
Akitoa
taarifa ya chanzo hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na
Usafi wa Mazingira (SUWASA) mjini Singida Hosea Maghimbi amesema zaidi
ya shilingi bilioni 1.5 sawa na asilimia 99.2 kwa kipindi cha mwaka wa
fedha wa 2016/17 kwa ajili ya fidia kwa wakazi walio jirani na chanzo
hicho.
Maghimbi
amesema SUWASA iko katika ujenzi wa mradi wa mtandao wa maji na mfumo
wa maji safi Singida mjini pamoja na kuboresha huduma ya maji kwa miji
midogo ya Manyoni na Kiomboi.
Amesema
baadhi ya changamoto zinazokabili SUWASA ni pamoja na wateja kutolipa
madeni kwa wakati hasa taasisi za serikali, wateja wanaokatiwa huduma
kwa sababu ya madeni kutorejeshewa huduma hizo na badala yake kununua
maji kwa majirani, kujifungia maji na kuchepusha dira za maji.
Maghimbi
ametoa wito kwa wananchi kutokata miti, kuchoma moto, kuchungia mifungo
na kufanya shughuli zangine za binadamu kwenye vyanzo vya maji.
“Nitumie
nafasi hii kuwaomba wananchi kufichua watu wanaojiunganishia maji
kiholela, wanaojifungia maji na kuchepusha dira ya maji, kwamba SUWASA
inatoa zawadi ya shillingi 50,000 kwa ye yote atakayetoa taarifa sahihi
kuhusiana na watu hao, ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria”,
amesema Maghimbi.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akijitwisha ndoo ya maji baada
ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama ikiwa
ni maadhimishi ya kilele cha wiki ya maji yaliyofanyika katika kijiji
hicho cha Iguguno, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Mkalama Injinia Jakson
Masaka.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa
kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama Bi Joyce ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia baadhi ya wananchi wa
kijiji cha Iguguno Wilaya ya Mkalama kwenye maadhimishio ya kilele cha
wiki ya maji. Pamoja na mambo mengine Dkt. Nchimbi ameagiza askari wa
usalama barabarani kupanda miti ya matunda ili waweze kula matunda
kuboresha afya za macho yao waweze kuona vizuri kipindi wanatekeleza
majukumu yao barabarani.
No comments:
Post a Comment