Wabunifu
wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na
Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye
sekta za ubunifu na biashara mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo
la kiserikali (Culture and Development East Africa -CDEA) la jijini Dar
es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na
masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ tawi la Afrika
Mashariki.
Awali
akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi
Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza
washiriki kwa kuchaguliwa kwenye mradi huo ambao ni wa kwanza na wa
kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika
kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao
kuzingatia yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko
nje ya mipaka ya nchi zao wanazotoka.
Mafunzo
hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika
kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo
zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria na mbinu tofauti za kupata
ufadhili. Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo
Bibi Santa Anzo na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza
kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo
kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika.
Washiriki
ambao ni wabunifu kutoka Afrika Mashariki akiwemo Andrew Kalema, Joyce
Gerald (katikati) na Makeke Jocktan wakifuatilia mafunzo hayo.
Washiriki
hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi
zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja
na kujitengenezea majinna (branding). Mafunzo hayo ya siku nne,
yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani
ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba ya
hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na simbi ambazo
zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi
zao hizo.
Kwa
upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia
kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo
wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo. Mradi huo pia
unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) unaratibiwa na CDEA
kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la kukuza ujuzi na elimu
ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa
sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na
Uganda.
Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa akitoa takwimu za fashionomics kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Kwa
sasa mafunzo hayo ya Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) yameanza na
masuala ya ubunifu wa mavazi na urembo ambapo pia yatafuatiwa na mafunzo
mengine ikiwemo Muziki na filamu. Mwisho. CODES: CDEA yaendesha mafunzo
ya IIDEA 2017 kwa wabunifu mavazi na urembo wa Afrika Mashariki
Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo
Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani
zao kwenye sekta za ubunifu na biashara IIDEA 2017,mafunzo
yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development
East Africa -CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi
na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa
na GIZ tawi la Afrika Mashariki.
Awali
akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi
Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza
washiriki kwa kuchaguliwa kwenye mradi huo ambao ni wa kwanza na wa
kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika
kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao
kuzingatia yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko
nje ya mipaka ya nchi zao wanazotoka.
Kemi Kalikawe kutoka Tanzania akipitia mchoro wa mshiriki Clare Musila (Uganda) wakati wa mafunzo hayo.
Mafunzo
hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika
kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo
zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria na mbinu tofauti za kupata
ufadhili. Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo
Bibi Santa Anzo na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza
kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo
kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika.
Washiriki
hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi
zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja
na kujitengenezea majinna (branding). Mafunzo hayo ya siku nne,
yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani
ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba ya
hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na simbi ambazo
zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi
zao hizo.
Kebirugi Nina akishona vazi alilobuni.
Kwa
upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia
kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo
wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo. Mradi huo pia
unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) unaratibiwa na CDEA
kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la kukuza ujuzi na elimu
ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa
sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na
Uganda.
Kwa
sasa mafunzo hayo ya Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) yameanza na
masuala ya ubunifu wa mavazi na urembo ambapo pia yatafuatiwa na mafunzo
mengine ikiwemo Muziki na filamu. Tazama hapa matukio mbalimbali ya
picha ya mafunzo hayo:
Washiriki na wataalamu wakibadilisha mawazo wakati wa semina magunzo hayo.
Bi Amal Mohamed kutoka Kenya akitoa mafunzo ya namna ya kupata Ufadhili kupitia ubunifu kwa wabunifu wa Afrika Mashariki.
Bi Bernadine Buzabo akiwasilisha mafunzo kwa washiriki kwa njia ya mtandao wa Skype kwa washiriki (Hawapo pichani).
Mmoja wa wanufaika wa ufadhili kupitia ubunifu kutoka Kenya Bwana James Otieno akitoa mafunzo kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki Ester Kiula na Whitnery Gnaj wakifuatilia mafunzo hayo.
Mshiriki kutoka Uganda, John Okello akishona vazi alilobuni mwenyewe wakati wa mafunzo hayo.
Mshiriki akimuonesha mkufunzi kazi yake namna ya inavyovaliwa.
Mshiriki akipata maelekezo ya vipimo toka kwa mkufunzi.
Kemi Kalikawe akimuelekeza Catherine Mood Board.
Mshiriki Victoria Joseph akiwa kwenye ubunifu wake
Whitney Gnaj akijaribu vazi alilolibuni
Kemi Kalikawe akipitia mchoro wa Clare Musila
Wakili
masuala ya miradi na biashara Bi. Sia Mrema akifundisha kuhusu usajili
wa biashara na makampuni kwa washiriki hao ili kujitangaza zaidi hasa
kupitia majina yao ya ubunifu (brand).
Bibi
Santa Anzo ambaye ni mbunifu mkongwe na mahiri nchini Uganda akitoa
mafunzo ya namna ya wabunifu watakavyoweza kubuni ubunifu wao na kuuza
bidhaa zao katika masoko ya nje.
Aliyewahi kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Bi. Nasreen Karim akipitia kazi ya mwanafunzi Clare Musila
Aliyewahi
kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Bi. Nasreen Karim akitoa mafunzo
kwa wabunifu hao (Hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya IIDEA 2017.
Mmoja wa walimu wakitoa mafunzo katika mafunzo hayo.
Vazi la mbunifu wa Tanzania Makeke Jocktan alilolibuni wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Wabunifu wakiendelea na ubunifu wao
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Kazi za wabunifu zilizofanywa na washiriki
Baadhi ya washiriki wabunifu na walimu wakipiga picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa.

إرسال تعليق