WATANZANIA
wamepata nafasi ya kuwakilisha Afrika Mashariki katika uwanja wa mpira
wa Anfield unaotumiwa na Liverpool baada ya timu iliyokuwa inawakilisha
ya Azania Group kutwaa ubingwa wa Standard Chartered 2017. Katika
michuano hiyo iliyohusisha klabu zilizoingia fainali kutoka Tanzania,
Kenya na Uganda mwakilishi wa timu ya Liverpool mchezaji gwiji John
Barnes na mabalozi wa Uingereza, Uganda na Kenya, Azania ilionesha
kandanda safi . Azania imepata nafasi ya kutwaa kombe hilo katika
Mashindano hayo ambayo yanajulikana kama ‘Standard Chartered-Road to
Anfield Tournament’ kwa tofauti ya magoli katika kipute ilichokipiga na
Capital FM katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es
Salaam jana.
Mwakilishi
wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande (kushoto) akiwasili kwenye
viwanja vya JK Youth Park na kupokelewa na Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa
Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (katikati) wakati wa
fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017
yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz)
Azania
Group of Companies ambayo ilikuwa inawakilisha Tanzania ilijikusanyia
pointi saba kama ilivyokuwa Capital FM kutoka Kenya lakini waliweza
kupata nafasi kutokana na kujipatia magoli matatu zaidi dhidi ya Kenya
ambao walikuwa na magoli mawili. Mpira huo ambao ulichezwa kwa dakika
tano kila upande ulikuwa mkali na ambao ulishindwa kutoa utabiri wa wazi
nani ataibuka mshindi na hivyo kupata nafasi ya kuingia uwanja wa
Anfield Mei mwaka huu kuangalia mechi za Liverpool. Baada ya kila timu
kuicheza mechi tatu katika raundi ya kwanza na kila mmoja kujipatia
pointi tatu waliingia katika raundi ya pili.
Mwakilishi
wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande (mwenye kofia) akizungumza na
timu ya Capital FM baada ya kuwasili kwenye viwanja vya JK Youth Park
jijini Dar es Salaam. Katika michuano hiyo Coca cola ya Uganda ilicheza
dhidi ya Azania Group of Companies na kuondolewa mapema katika michuano
hiyo pamoja na watu wake kuwa na miili ya soka. Kutokana na Uganda
kuondolewa mapema, Azania waijikuta wakikabiliana na washindi wa mwaka
uliopita mabingwa wa Kenya. Kenya walicheza mpira ambao ulileta taabu
sana, mpira wa kujihami na hivyo kutibua mbinu waliyokuwa nayo Azania
ambao walitaka kumaliza game mara moja. Unaweza kusema kwamba kipa wa
Capital FM’s, Shafi Sudi ndiye alikuwa staa wa mechi kutokana na
kufanikiwa kuzuia kasi ya mashambulizi kutoka Azania yaliyokuwa
yakiongozwa na Nahodha Shabaka Hamis.
Balozi
wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha (mwenye tisheti nyeupe)
akizungumza na timu ya Coca cola kutoka Uganda mara baada ya kuwasili
kwenye viwanja vya JK Youth Park kushuhudia fainali za mashindano ya
Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyomalizika jana jijini Dar
es Salaam.[/caption] Kutokana na fainali hizo kutokuwa na mfumo wa
penati timu ambayo inamaliza gemu ikiwa na pointi zaidi huwa ndio
washindi na katika hilo Watanzania ndio wawakilishi wa timu za Afrika
Mashariki katika uwanja wa Anfield. Kutokana na ushindi huo Capital FM
wanakuwa wa pili na nafasi ya tatu inashikwa na Coca cola ya Uganda.
Akizungumza baada ya gemu kumalizika, Rajab Ali ambaye ndiye aliyeibeba
Azania Group alisema kwamba alikuwa na furaha kubwa kwenda kuishuhudia
Liverpool FC ikikipiga katika uwanja wa Anfield kwani ndilo ilikuwa nia
yao kubwa.
Gwiji
wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes
(katikati) akiwasili pamoja na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard
Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) na kupokelewa na Mkuu wa
Uhusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba walipowasili kwenye
viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.[/caption] Naye nahodha
wa Capital FM, Lassie Atrash alisema kwamba wameshindwa kufanya vyema
kwa kuwa uwanja ulikuwa mdogo. Hata hivyo alisema ulikuwa ni mchezo safi
na mshindi ilikuwa lazima apatikane na kusema kwamba ana matumaini kuwa
Azania itawawakilisha vyema Afrika Mashariki huko England. Awali
mchezaji John Barnes akizungumza kabla ya michezo hiyo alisema
anafurahishwa na kutambua kwamba soka linatengenezwa Afrika Mashariki na
hivyo kuondoa dhana potofu kwamba soka katika Afrika linapatikana
Afrika magharibi pekee.
Gwiji
wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes
akitambulishwa kwa Mwakilishi wa Balozi wa Uingereza, Daniel Rathwell
alipowasili kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita
Mramba.[/caption] Alisema kwamba amefurahishwa na kuona kwamba Liverpool
imepata mashabiki wengi kutoka Afrika ambao wanatengeneza familia ya
timu hiyo katika sera iliyoanzishwa miaka ya 1960 ya kuwa na wapenzi na
mashabiki wa damu wa timu hiyo. Aidha alizungumzia uhusiano wao na
walezi Standard Chartered na kutabiri kwamba Tanzania itaibuka washindi
kutokana na yeye kuwapo Kenya mwaka uliopita na Kenya kufanikiwa kwenda
England kuishuhudia Liverpool. Pamoja na mchezaji huyo mahiri wa zamani
wa Liverpool kuzungumza katika fainali za tuzo hizo, wapenzi wa michezo
pia walipata kusikia nasaha kutoka kwa Balozi wa Uingereza nchini,
Balozi wa Uganda na mwakilishi wa Kenya.
Meza
kuu kwenye fainali za mashindano ya Standard Chartered Road to Anfield
2017, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine, Mwakilishi wa Balozi wa Uingereza,
Daniel Rathwell, Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini
Uingereza, John Barnes, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered
nchini, Sanjay Rughani, Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali
Hyuha pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande.
Gwiji
wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes
akiwasalimia washiriki wa fainali mashindano hayo ya Standard Chartered
road to Anfield 2017 yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.
Timu ya Coca cola Uganda ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza fainali za mashindano hayo.
Timu ya Capital FM kutoka Kenya ikiimba wimbo wa Taifa kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Kikosi
cha timu ya Azania Group of Companies wakiimba wimbo wa taifa kabla ya
kuanza fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017
zilizofanyika kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kulia) akishiriki
kuimba wimbo wa taifa na vijana wake kabla ya kuanza kwa fainali za
mashindano hayo.
Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha katika picha ya pamoja na timu ya Coca cola kutoka nchini Uganda.
Meza kuu ikisalimiana na wachezaji na kuwatakia kheri ya mchezo mwema.
Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande katika picha ya pamoja na timu ya Capital FM kutoka Kenya.
Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akijumuika
na wadau wa soka kupasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mechi za
fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika
viwanja vya JK Youth Park.
Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia)
akibadilishana mawazo na Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool
nchini Uingereza, John Barnes wakati wa fainali za mashindano ya
Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyofanyika jana jijini Dar es
Salaam katika viwanja vya JK Youth Park.
Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akizungumza
na wageni waalikwa pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya
Standard Chartered road to Anfield 2017.
Mwakilishi
wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande akitoa salamu kwa washiriki wa
fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika
viwanja vya JK Youth Park.
Balozi
wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha akiwasalimu washiriki wa
fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika
viwanja vya JK Youth Park.
Mwakilishi
wa Ubalozi wa Uingereza, Daniel Rathwell akizungumza kwa niaba ya
balozi wake kwenye fainali za mashindano ya Standard Chartered road to
Anfield yaliyofanyika katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es
Salaam
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine,
akitoa salamu za TFF kwa wageni waalikwa na washiriki wa fainali za
mashindano hayo.
Wafanyakazi wa Standard Chartered Bank na wadau wa soka waliohudhuria fainali za mashindano hayo.
Mtendaji Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kulia) akitazama vijana wake walipokuwa uwanjani.
Benji la ufundi la Azania Group of Companies.
Mechi
ya utangulizi kati ya mashabiki wa timu ya Liverpool (tisheti nyeupe)
na wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered (vesti nyekundu) ambapo
mashabiki wa timu ya Liverpool waliinyuka benki hiyo bao 1-0.
Kiungo wa timu ya Azania Group of Companies, Rajabu Ali akiwatoka wachezaji wa timu ya Coca cola kutoka Uganda.
Nahodha
wa Capital FM, kutoka Kenya, Lassie Atrash akizungumzia mchezo
ulivyokuwa kwa wanahabari mara baada ya fainali hizo kuisha na Tanzania
kuchukua ubingwa.
Mbunge
wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda (kulia) na watoto wake katika picha ya
pamoja na Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini
Uingereza, John Barnes kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es
Salaam.
Mashabiki wa Liverpool wakiimba wimbo "You'll never walk alone" pamoja na Gwiji huyo John Barnes.
Mbunge
wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (katikati) akikabidhi zawadi kwa mmoja
wa waamuzi wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to
Anfield 2017 yaliyofanyika jana katika viwanja vya JK Youth Park jijini
Dar. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini,
Sanjay Rughani akiushuhudia tukio hilo.
Mwakilishi
wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande akiwavisha medali washindi
watatu timu ya Coca cola ya Uganda katika mashindano ya Standard
Chartered road to Anfield 2017. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya
Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akiushuhudia tukio hilo.
Picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo.
Balozi
wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha akiwavisha medali washindi
wa pili wa Standard Chartered road to Anfield 2017 timu ya Capital FM
kutoka Kenya. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered
nchini, Sanjay Rughani (wa pili kushoto) na Mkuu wa Uhusiano na Masoko
wa benki hiyo, Juanita Mramba wakiushuhudia tukio hilo.
Picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo.
Picha ya pamoja na washindi wa pili wa mashindano hayo timu ya Capital FM kutoka Kenya.
Mchezaji
maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes akimvisha medali
Nahodha wa Azania Group, Shabaan Hamis baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa
2017. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini,
Sanjay Rughani.
Mchezaji
maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (kulia) akikabidhi
kombe kwa timu ya Azania Group of Companies kutoka Tanzania, ambao ni
mabingwa wa mashindano ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017
jijini Dar es Salaam jana.Pamoja naye ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa
Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) na Mtendaji Mkuu
wa benki hiyo Sanjay Rughani (aliyezibwa).
Mchezaji
maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (katikati)
akiselebuka pamoja na wachezaji wa timu ya Azania Group kutoka Tanzania,
mara baada ya kuikabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya Benki ya
Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 jijini Dar es Salaam jana.
Pamoja naye ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki ya Standard
Chartered, Juanita Mramba (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo
Sanjay Rughani (aliyezibwa).
Mchezaji
maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (katikati) akifurahi
pamoja na viongozi na wachezaji wa timu ya Azania Group kutoka Tanzania
(walioko mstari wa nyuma) mara baada ya kuikabidhi kombe la ubingwa wa
mashindano ya Benki ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017
jijini Dar es Salaam jana.Wengine pichani ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko
Juanita Mramba (wa pili kushoto), Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sanjay
Rughani (wa tatu kushoto), Balozi wa Uganda nchini Mh. Dorothy Hyuha,
(wanne kushoto) na Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda na Mtendaji
Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kushoto).
Abdullah Zulu Lyana (katikati) katika picha ya pamoja na mashabiki wenzake wa timu ya Liverpool.
Post a Comment