Na. Lilian Lundo-Dodoma
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
ameziagiza Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo
kwa ajili ya wananchi kufanya mazoezi na kupumzika.
Kassim
Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Mjini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa
Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika katika
uwanja vya Jamhuri.
"Ni
muhimu kufanya mazoezi kila siku, mazoezi yanasaidia kuchangamsha
mwili, kufahamiana, kujenga urafiki pamoja na kuwa na afya bora,"
alisema Mhe. Majaliwa.
Waziri
Mkuu amesema kwamba, muitikio wa ufanyaji mazoezi wa viungo ni mkubwa,
ambapo watu wengi wamejiunga na vikundi mbalimbali vya kufanya mazoezi
ya viungo.
Aidha, amezitaka Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya watu kufanya mazoezi na kumpuzika.
Ameongeza
kuwa, watu wasilazimishwe kufanya mazoezi bali iwe ni hiari ya yao na
kusiwe na gharama kwa ajili ya mtu kufanya mazoezi.
Vile
vile amewataka Maafisa Utamaduni na Michezo nchini kuhamasisha mazoezi
ya viungo katika maeneo yao pamoja na kuanzisha vikundi vya mazoezi ya
viungo ambapo watakuwa wanakutana na kufanya mazoezi kwa muda ambao
watajipangia.
Kwa
upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwa kuhamasisha mazoezi ya viungo na kuitangaza rasmi Jumamosi ya
pili ya kila mwezi kuwa ni siku ya mazoezi ya viungo Kitaifa.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, mazoezi ya viungo yanamuepusha mtu na kupata magonjwa
yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo, kisukari pamoja na saratani.
Naye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amesema
kwamba, mazoezi ya viungo yanaratibiwa na Wizara ya Habari, Wizara ya
Afya pamoja na TAMISEMI. Hivyo kwa pamoja watahamasisha uanzishwaji wa
vikundi vya mazoezi ya viungo katika Halmashauri zote nchini kwa kuanza
na watumishi wa Umma.
Aidha
amewataka viongozi wanapokuwa mikoani katika siku ya mazoezi ya viungo
wawahamasishe wananchi kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kulinda
afya zao.
Uzinduzi
wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo ulianza kwa matembezi yaliongozwa na
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuanzia viwanja vya Bunge na
baadaye alimkabidhi Waziri Mkuu kuanzia Nyerere Square mpaka Uwanja wa
Jamhuri. Uzinduzi huo umehusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri,
Wabunge, Viongozi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wananchi wa Mkoa huo.
|
No comments:
Post a Comment