Mwandishi Wetu,Arusha
Wasomi
nchini wamepongeza uteuzi wa majaji wawili wanawake wa Mahakama ya Afrika na
Haki za Binadamu(AfCHPR)uliofanywa na Wakuu wa Umoja wa Afrika(AU) katika mkutano
wa 28 uliofanyika nchini Ethiopia kuwa unaelenga kujenga usawa wa kijinsia
katika chombo hicho cha maamuzi.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine
ulipitisha majina ya majaji wawili ambao ni Jaji Bensaoula Chafika kutoka
Algeria na Jaji Chizumila Rose Tujilane wa Malawi ambao wataitumikia mahakama
hiyo kwa kipindi cha miaka sita ijayo.
Majaji
hao wanachukua nafasi zilizoachwa wazi na Jaji Fatsah Ouguergouz(Algeria) na
Jaji Duncan Tambala(Malawi)ambao utumishi wao ulikoma tangu Septemba 5,2016.
Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial(Sekomu),Dk Happiness
Rwejuna aliyewaongoza wanafunzi wa sheria kutembelea Mahakama hiyo yenye
makao yake jijini hapa alisema uamuzi uliofanywa na AU ni mzuri na ufaa
kuigwa na nchi wanachama katika uteuzi wa wanawake wenye uwezo katika nafasi
za maamuzi.
“Naamini
idadi ya wanawake wenye elimu ya juu wapo wengi na wanaweza kufanya kazi kwa
umahiri mkubwa,isihishie katika ngazi ya AU tuu bali ishuke hadi kwa nchi
moja moja kuona wanawake wana mchango muhimu katika maendeleo ya Afrika kwa
ujumla,”alisema
Majaji
hao wanatarajiwa kuapishwa katika kikao cha 44 kinachotarajiwa kufanyika
Machi 6,2017 jijini Arusha ikiwa ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kuwa na
majaji wanawake watano katika majaji 11 wa mahakama hiyo tangu ianze kazi
zake mwaka 2004.
Naye
Emmanuel Chipanta mwanafunzi wa mwaka tatu alisema uwepo wa mahakama hiyo una
umuhimu katika kuimarisha utawala sheria kwani kumekua na makosa mengi
yanayotendeka ambayo wahusika hawana budi kukabiliana na mkondo wa sheria.
Alisema
uwiano wa kijinsia unatajwa katika itifaki iliyoanzisha mahakama hiyo katika
ibara ya 12(2) na Ibara ya 14(3).
Kwa
upande wake Mwanasheria wa Mahakama hiyo,Selemani Kinyunyu wakati akijibu
hoja za wanafunzi hao waliotaka kufahamu uamuzi wan chi za Afrika kutaka
kujiondoa katika Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai alisema sula hilo
lina sura mbili katika nchi zinazotaka kujiondoa na zinazotaka kubaki.
“Zipo
nchi zinazoona mahakama hii imekua ikiwalenga viongozi wa Afrika zaidi badala
ya kushughulikia jinai ulimwenguni kote hivyo kuona hamna sababu ya kuendelea
kuwa mwanachama,laikini wapo wanaodhani ni muhimu kuendelea kuwepo ili kuotoa
mapendekezo ya maboresho pale penye mapungufu jambo ninaloliunga mkono,”alisema
No comments:
Post a Comment