Benny Mwaipaja, WFM, Kyela
UJENZI
wa meli mbili za mizigo katika Bandari ya Itungi wilayani Kyela Mkoani
Mbeya, MV Njombe na MV Ruvuma, umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98 na
kwamba meli hizo zinatarajiwa kufanyiwa majaribio Ziwa Nyasa, mwishoni
mwa mwezi Februari na kukabidhiwa rasmi Serikalini mwezi Machi, 2017
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Songoro MarineTransport Ltd ya Jijini Mwanza,
inayounda meli hizo, Mhandisi Saleh Songoro, amesema hayo wakati ujumbe
wa Serikali ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizaya ya Fedha na
Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea Bandari hiyo ukiwa
katika zaira ya kukagua hali ya biashara mipakani mkoani Mbeya.
Amesema
kuwa kukamilika kwa meli hizo mbili za mizigo za kisasa zenye uwezo wa
kubeba tani elfu moja (1,000) za mizigo kila moja na kugharimu shilingi
bilioni 11, kutaiwezesha Kampuni hiyo kuanza kuunda meli nyingine ya
tatu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo.
Pamoja
na meli hizo, Mhandisi Songoro amesema kuwa mradi huo pia umewezesha
kujengwa kwa cherezo cha kwanza na cha pekee kitakacho iwezesha Mamlaka
ya Bandari Tanzania-TPA katika uundaji wa meli na kuzifanyia matengenezo
meli nyingine za ndani na nje ya nchi zikiwemo Malawi na Msumbiji.
Kaimu
Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bandari ya Itungi, Bw. Ajuaye
Msese, amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kuunda meli hizo ulikuwa
kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa vyombo vya baharini vya
kusafirisha abiria na mizingo ndani na nje ya nchi kupitia Ziwa Nyasa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango, , pamoja na kupongeza kazi kubwa iliyofanywa
na mkandarasi mzawa, Songoro Marine Transport Ltd, kuunda meli hizo,
wamesema kuwa kukamilika kwa meli hizo kutachochea biashara na mapato ya
serikali kupitia shughuli za usafiri na usafirishaji katika Ziwa Nyasa.
Prof.
Mkenda amesisitiza kuwa Serikali itaangalia uwezekano namna ya kumtumia
Mkandarasi huyo, Bw. Saleh Songoro, kuunda meli nyingi zaidi za ndani na
nje ya nchi ili kukamata soko hilo la utengenezaji wa meli kitaifa na
kimataifa hatua itakayoliletea Taifa sifa, kukuza uwekezaji na ajira.
Ujenzi
wa Meli zote tatu, mbili za mizigo pekee, na moja ya mizigo na abiria,
umekadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 20 na utakuwa
umetekeleza ahadi ya Serikali ya muda mrefu ya kuboresha usafiri wa
abiria na mizigo kupitia Ziwa Nyasa, ambapo unatarajiwa kukuza biashara
kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji, kusisimua uchumi wa wakazi wa
wilaya ya Kyela na ukanda wote wa Kusini.
Aidha
kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo kutapunguza matukio ya ajali za mara
kwa mara zinazogharimu maisha ya watu wengi wanaotumia Ziwa Nyasa,
linalo tajwa kuwa la pili kwa kuwa na mawimbi makali na la tano kuwa na
kina kirefu cha maji duniani.
Meli
mbili za Mv. Ruvuma na Mv Njembe zikiwa katika cherezo katika Bandari ya
Itungi, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, zikiwa katika hatua za mwisho
kabla ya kuanza kufanyiwa majaribio ndani ya Ziwa Nyasa Mwishoni mwa
Februari, 2017.
Bw.
Juma Nassoro akipaka rangi meli ya mizigo ya Mv Ruvuma, ikiwa ni hatua
za mwisho wa ukamilishaji wa uundaji wa meli hiyo yenye uwezo wakubeba
tani 1000 za mizigo itakayokuwa ikifanya safari zake Ziwa Nyasa, wakti
Ujumbe wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda
Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ulipofanya
ziara katika Bandari ya Itungi, wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Kaimu
Mkuu wa Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, Bw. Ajuaye Msese
akitoa maelezo mafupi kuhusu Bandari ya Itungi, na majukumu yake kwa
ujumla kwa wageni waliotembelea Bandari hiyo mkoani Mbeya.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd, inayounda meli
tatu katika Bandari hiyo, Bw. Saleh Songoro, akielezea historia fupi ya
kampuni yake iliyoingia mkataba na Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA
kuunda meli tatu Ziwa Nyasa, baada ya Ujumbe wa Serikali ukiongozwa na
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban,
ulipotembelea Bandari hiyo wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha
mchoro wa meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 kila moja
anazoziunda kwa ajili ya matumizi katika Ziwa Nyasa, katika Bandari ya
Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, baada ya kutembelewa na ujumbe wa
Serikali unaofuatilia masuala ya biashara mipakani mkoani Mbeya.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha
moja kati ya ya meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000
kila moja anazoziunda kwa ajili ya matumizi katika Ziwa Nyasa, katika
Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, baada ya kutembelewa na
ujumbe wa Serikali unaofuatilia masuala ya biashara mipakani mkoani
Mbeya.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro,
akionyesha mchoro wa meli mbili za mizigo za MV Ruvuma na Mv Njombe
alizoziunda wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi.
Amina Khamis Shaaban (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani Balozi Hassan Simba Yahya (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa tatu
kushoto) walipozulu Bandari ya Itungi, iliyoko Wilayani Kyela mkoani
Mbeya.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akiongoza
ujumbe wa Serikali kutoka Wizara za Fedha, Uwekezaji, na mambo ya Ndani
kujionea kazi ya ujenzi wa Meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba
tani 1000 za mizigo kila moja zinazojengwa katika Bandari ya Itungi
iliyoko Wilayani Kyela mkoani Mbeya
Mkurugenzi
Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha
mfumo wa kuongoza meli katika chumba cha nahodha wa meli ya Mv Njombe,
huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biasha na Uwekezaji Prof Adolf.
Mkenda, akiangalia kwa makini mfumo huo wa kisasa namna unavyofanya
kazi.
Baadhi
ya wajumbe wa Serikali waliofanya ziara katika Bandari ya Itungi mkoani
Mbeya kujionea uundwaji wa meli mbili za mizigo wakishuka kwenye ngazi
baada ya kumaliza kukagua meli ya Mv Njombe inayotengenezwa na Kampuni
ya Songoro Marine Transport Ltd inayoshughulika na kutengeneza vyombo
vya usafiri vya majini katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoani
Mbeya. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
No comments:
Post a Comment