Na Zainab Nyamka,
Globu ya Jamii
Globu ya Jamii
Kampuni ya Trumark inayofanya mafunzo ya kuboresha ufanisi katika
jamii imefanya mafunzo ya kujitoleta kwa kuwapatia Elimu ya kuwawezesha
Wanawake Kiuchumi katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo ambaye pia ni Balozi wa
Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Duniani kupitia Umoja wa Mataifa alisema
kuwa ni muhimu vijana kutafuta na kukamata fursa mbalimbali kutoka
kwenye jamii yao. Ikiwa ni pamoja na kujitolea kupitia vipaji vyao
husuani elimu ili kuweza kuitumikia jamii.
Warsha hii iliyolenga kutimiza moja ya majukumu ya kuwa Balozi wa
Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi iliambatana na kutoa shuhuda mbalimbali za
mafanikio, elimu na ajira huku wakiwajengea wanafunzi wa chuo hicho
uwezo wa kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka katika jamii yao.
Mafunzo haya yalihimiza nguvu na matumizi sahihi ya mitandao ya
kijamii. Bi Agnes aliongeza kwa kusema kuwa mitandao ya kijamii ni
mizuri hasa unapoamua ikuletee mafanikio katika maisha.
Jukwaa la Kimataifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi lina washiriki
kutoka nchi 198, watazamaji 900,000, washiriki 18,500 na mabalozi 410
duniani kote.
Bi Agnes aliwashukuru Kampuni ya Kisima kwa kuweza kutambua umuhimu
wakuwapatia vijana fursa nakuwezesha kufanikisha warsha hii muhimu. Na
shukrani nyingine alizielekeza kwa uongozi wa chuo cha Ustawi wa Jamii
cha Dar es Salaam kwa kuruhusu kutumia chuo cha kama jukwaa la kuwapatia
elimu hii muhimu wanafunzi wa chuo hicho.
Tunategemea kufikia vijana wengi zaidi ili nao waweze kuwa mabalozi
wazuri wa kuwawezesha wanawake kiuchumi hususan kwa nchi yetu ya
Tanzania.
Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Muwezeshaji
na Balozi wa Vijana kutoka East Community Youth Ambassador Platform
Kamala Dickson akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii
wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Afisa
habari wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Stella Vuzo akizungumza na
wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha
Wanawake Kiuchumi.
Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii wakijiandikisha wakati wa semina ya kuwapatia Elimu ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa TruMark Bi Agnes Mgongo akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji
wa semina hiyo waliokaa na wanafunzi wa chuo cha ustawi wa Jamii.Picha na Zainab Nyamka.
No comments:
Post a Comment