Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kifurishi kisicho isha muda cha halichachi. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
KAMPUNI ya Tigo Tanzania leo imetangaza kuanzishwa kwa ubunifu mwingine wa kifurushi cha data na sauti ili kukabiliana na hitaji la wateja. Kifurushi kipya kinajulikana kama ‘Halichachi’ (Muda wake hauishi) na ni mwendelezo wa kujikita kwa Tigo katika kuwapatia wateja wake uhuru wa mawasiliano.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo wakati akitangaza kampeni hiyo mpya Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga alisema, “Tuna furaha kubwa wakati kampuni inazindua kifurushi kipya ambacho kitawahakikishia wateja wake kwamba wanakuwa na mamlaka ya kumiliki vifurushi vyao wakati muda wa kumalizika kwa kifurushi haitakuwa ni changamoto tena.”
“Ni dhahiri kuwa soko la mawasiliano ya simu linakua ambapo huduma za mawasiliano ya simu za mkononi zinaongezeka kwa mrengo wa kununua vifurushi,” alisema Mpinga na kuongeza, “Tunazindua kifurushi cha kipekee tukiwa tunajiamini kwamba kitakuwa ni suluhisho sahihi kwa wateja wetu.
“Kifurushi hiki kinaingia katika soko ikiwa ni sehemu ya mtiririko wa ubunifu uliowekwa ili kuhakikisha kwamba tunasimamia mtazamo wetu katika kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu.
Tunaamini kwamba kifurushi hiki ni kiashiria kilicho wazi kwamba tunaongoza katika kutoa masuluhisho ya mawasiliano ya simu yaliyo na ufanisi nchini Tanzania.”
Kifurushi hiki kipya ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kutoa huduma ndani ya safari yake ya ubunifu na miongoni mwake ikiwa ni kuanzishwa kwa huduma ya bure ya WhatsApp, Facebook ya Kiswahili na YouTube ambayo kampuni ilizindua mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment