Hussein Makame, NEC aliyekuwa Bukoba
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imewatahadharisha watu wanaochukua kadi za kupigia
kura za wenzao na kuzizuilia au kubaki nazo kuwa ni kinyume cha Sheria.
Hayo
yamesema na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika
halmashauri ya manispaa ya Bukoba na Shinyanga hivi karibuni.
Alisema
kifungu cha 88 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinasema kuwa ni kosa la
jinai kwa mtu kuchukua kadi ya mpiga kura mwingine na kuiziulia,
kukataa kuirudisha au kubaki nayo kwa uzembe.
Bw.
Kawishe alifafanua kuwa kumekuwa na malalamiko kwamba inapofikia karibu
na kipindi cha uchaguzi, baadhi ya watu wanachukua kadi za wapiga kura
wengine na kuzizuia kinyume cha Sheria.
Hata,
hivyo alisema kutokana na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia mikutano na
kuhudhuria maonesho mbalimbali, baadhi ya wananchi wameelewa umuhimu wa
kadi hizo na kuahidi kutoampa mtu kadi zao za kupigia kura.
“Kwa
hiyo katika jambo hilo tumekuwa na mrejesho ambo ni chanya lakini
tunachowaomba ukiandikishwa tunza kadi yako ya mpigia kura” alisema Bw.
Kawishe na kuongeza kuwa;
“Jambo
la pili mwananchi usikubali mtu achukue kadi yako ya mpigia kura na
wala usitumie kadi yako ya mpiga kura kwenye kuchukulia dhamana sehemu
yoyote”
“Kwa
sababu itakwenda kuchukulia dhamana alafu utashindwa kwenda kupiga kura
unapofika wakati wa kupiga kura, mwananchi ajue kwamba kupiga kura ni
haki yake”
Alisema
mtu aliyejiandikisha asipokwenda kupiga kura anakosa haki ya kuchagua
kiongozi anayemtaka na badala yake anawaacha wenzako wakuchagulie
kiongozi.
“Unaacha
kupiga kura alafu baadaye anakuja kulalamika unasema huyu kiongozi
simtaki kumbe kura moja inatosha kubadilisha matokeo ya eneo zima”
alisema.
Hivyo
aliwasihi wananchi waendelee kuzingatia amani katika uchaguzi na
kuwashukuru kwa jinsi uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na uchaguzi mdogo
uliofanyika Januari 22 mwaka huu kwa jinsi ulivyokuwa na amani na
utulivu.
”Kwa
kweli Watanzania tutambue kuwa amani ni yetu sisi sote na sisi ndio
tutakaoilinda hiyo amani tuiweke Tanzania yetu kwanza alafu sisi
baadaye” aliwakumbusha Watanzania.
Akijibu
swali la mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bukoba aliyehoji
anayepoteza kadi ya mpiga kura anachukuliwa hatua gani kumuwajibisha,
Bw. Kawishe alisema hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yake.
Alifafanua
kuwa wale wote wanaopoteza kadi ya mpiga kura wanatakiwa wafike kwenye
kituo cha uboreshaji wa daftari la wapiga kura na kujieleza na
watapatiwa kadi nyingine.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia)
akisalimiana na mwenyeji wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Kanda ya Shinyanga Jaji Richard Kibelabaada ya mwenyeji wake kumpokea
wakati akiwasili mkoani Shinyanya kutoa Elimu ya Mpiga Kura
mkoani humo.Kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga
Sekela Mwaiseje.
Mkurugenzi
waHuduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe,
akisamiliana na Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bw.
Geofrey Ramadhani Mwangulumbi baada ya kuwasili kwenye Halmashauri hiyo
kutoa Elimu ya Mpiga kura.
Mkurugenzi
waHuduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe,
akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati
alipomtembelea ofisini kwake mkoani humo.
Mkurugenzi
waHudumaza Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel
Kawishe akitoa Elimu ya Mpiga kurakupitia Kituo cha redio Faraja Fm cha
mkoani Shinyanga mwishoni mwa wiki hii.Kulia kwake ni mtangazaji wa redio
hiyo Faustin Kasala.
Mkurugenzi
wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel
Kawishe, akitoa Elimu ya Mpiga kura kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari
ya Old Shinyanga iliyopo manispaa ya Shinyanga.Picha na Hussein Makame, NEC.
No comments:
Post a Comment