Marehemu Anorld Swai enzi za Uhai wake
WATU saba wamepoteaza maisha papo hapo katika
tukio la ajali ya barabarani iliyotokea leo jioni katika eneo la Mwika mpakani
mwa Wilaya ya Rombo na Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro.
Waliopoteza maisha ni pamoja na Mwandishi wa gazeti
la Habarileo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Hai, Anorld Swai.
Akizungumza na Daily News-Habarileo Blog, Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,SACP,Wilbroad Mutafungwa alithhibitisha kutokea
kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali ilitokea majira ya saa 11 jioni ikihusisha
magari mawili na pikipiki maarufu kama Bodaboda.
“Ajali imetokea majira ya saa 11 jioni ambapo
watu saba wamepoteza maisha wanne ni kutoka katika Toyota Surf T606 AQZ, mmoja
katika bodaboda MC 101 ANC huku wengine wakiwa ni kwenye Fuso T343 BNL,”alisema
Kamanda Mutafungwa.
Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la
Mwika katika Kijiji cha Mawanjeni katika mpaka wa Wilaya ya Rombo na Wilaya ya
Moshi Vijijini na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo inaweza kuwa ni kuharibika
kwa mfumo wa Breki wa Fuso iliyokuwa imebena ndizi ikitokea Rombo kwenda Jijini
Dar es Salaam.
Mbali na Swai wengio waliopoteza maisha na
kutambulika ni Mjumbe wa NEC ya CCM na Katibu wa CWT kutoka Same Ally Mbaga, Mwenyekiti
wa UWT Anastazia Malamsha, Edwin Msele, Mwanafunzi wa mwaka wanne Chuo cha KCMC.
Majeruhi wa ajali hiyo ni Jackson Kimambo -
Mwandishi gazeti la Nipashe -
amekimbizwa Hospitali ya KCMC kwa Matibabu pamoja na Mwendesha Bodaboda.
No comments:
Post a Comment