Usiku
wa February 5 ndio siku ambayo mchezo wa fainali ya mataifa ya Afrika
maarufu kama AFCON 2017 ulichezwa, mchezo wa fainali ya AFCON 2017
ulikuwa unazikutanisha timu za Misri dhidi ya Cameroon, lakini Cameroon
wamefanikiwa kufuta uteja kwa kufungwa fainali mbili na Misri.
Cameroon
wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, Nicolas N’koulou alifunga goli
la kusawazishia Cameroon dakika ya 58 baada ya Mohamed Elneny kuifungia
Misri goli la uongozi dakika ya 22, Vincent Aboubakar ndio alizima
ndoto za Misri baada ya dakika ya 88 kufunga goli la ushindi.
Ushindi
huo unakuja baada ya Cameroon kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri,
alifungwa fainali ya AFCON 2008 goli 1-0 Mohamed Aboutrika akifunga
goli hilo, lakini walipoteza fainali ya AFCON 1986, Cameroon wanakuwa
wamechukua taji lao la tano la AFCON wakati Misri wanabakia na rekodi
yao ya kuchukua mataji nane ya AFCON.
Rekodi
nyingine zilizowekwa katika AFCON na Cameroon ni kuwa inakuwa timu ya
kwanza kuwahi kuifunga Misri goli katika fainali za AFCON baada ya
Ethiopia, huku kocha wa Misri Hector Raul Cuper akiendeleza rekodi yake
mbovu kwa kupoteza fainali yake ya sita katika soka akiwa kama kocha wa
timu tofauti.
No comments:
Post a Comment