Na Nteghenjwa Hoseah, Karatu
MKUU
wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya
Karatu, Theresia Mahongo kuhakikisha fedha za walimu wa shule za
sekondari na msingi zilizokatwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwaajili
ya vitambulisho vya kazi zinarudishwa.
Mhe.
Gambo alitoa agizo hilo jana wilayani Karatu wakati alipokuwa
akizungumza na walimu hao kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Karatu
Boys
ili kujua changamoto wanazokutana nazo na jinsi ya kuzitatua ikiwemo
madeni ya likizo, upandaji wa madaraja.
Alihoji
ni kwanini walimu hao wakatwe Sh. 6000 kwa ajili ya kutengenezewa
vitambulisho vya kazi wakati ni haki yao kama watumishi na waajiriwa wa
halmashauri hiyo na ni haki yao kupata vitambulisho vya kazi bure;
Mwajiri anao wajibu wa kumtengenezea kila mtumishi Kitambulisho cha
kazi.
Alimwagiza
DC Mahongo kuhakikisha anafuatilia na kumchukulia hatua watumishi wa
halmashauri hiyo waliowakata walimu hao wa msingi na sekondari kiasi
hicho cha fedha kwa ajili kuwachukulia hatua.
"Eti
vitambulisho vyenu mmetozwa hela kwa sababu gani wakati ni bure... Sasa
nasema aliyehusika na kuwatoza Sh, 6000 kwa ajili ya vitambulisho vyenu
vya kazi atachukuliwa hatua kwa nini muwafanye walimu kama shamba la
bibi? Hamuwaonei huruma jamani? Wanadai malipo yao na hata vitambulisho
vya kazi pia muwakate hela zao hii siikubali"
Pia
Mhe. Gambo aliwaondoa hofu walimu hao kuwa serikali ya mkoa wa Arusha
itahakikisha kuwa madeni yote yanayodaiwa na walimu hao yatashughulikiwa
ili waweze kufundisha vyema wanafunzi wao.
Awali
walimu hao baadhi walisema wengine wanatembea umbali mrefu kwa ajili ya
kutoa elimu huku wanafunzi nao kwenye baadhi ya shule wakishindwa
kuhudhuria masomo yao kwa wakati sababu njiani wanakutana na
wanyamapori.
Pia
Mwalimu Joachim Petro akisema awali alisimamishwa kazi kwa mizengwe na
baadaye kurudishwa kazini na kuamriwa kupewa Shilingi milioni 3. 5 kama
madai ya usumbufu na mshahara yake lakini tangu mwaka juzi hajapewa
fedha zake
Pia
fedha za walimu za SACCOS zaidi ya Sh. milioni 11.3 za walimu ambazo ni
makato yao hawazioni na hata wakitaka kuzikopa wanaelezwa hazipo sasa
zimekwenda wapi.
Awali,
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mahongo alisema anafuatilia suala hilo ili
kujua ni mtumishi gani wa halmashauri alichukua fedha hizo kwa
kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Bw.
Waziri Morice ili kuchukua hatua kali za kinidhamu.
No comments:
Post a Comment