Na Mwandishi wetu.
Kufuatia
kuungua kwa mara ya pili kwa soko kuu la kayanga katika Halmashauri ya
Wilaya ya Karagwe, Ofisi ya Mkuu wa mkoa Kagera imeiagiza Halmashauri
hiyo kuunda timu mara moja na kuanza uchunguzi wa chanzo cha moto huo
katika soko hilo, ambalo kwa mara ya kwanza liliungua tarehe 11 Machi,
2016.
Sehemu
ya soko kuu la Kayanga imeungua usiku wa kuamkia tarehe 7 Januari,
2017, saa 9:00 usiku, ambapo vibanda 52 vilivyojengwa kwa mbao na meza
24 za wafanyabashara wadogowadogo wa nafaka, matunda na mbogamboga
vimeteketea kwa moto pamoja na mali za wamachinga waliokuwa wanapanga
chini wapatao 33 nao mali zao zimeteketea kwa moto.
Akiongea
mara baada ya kukagua athari za janga la moto katika soko hilo Katibu
tawala wa Mkoa wa Kagera Kamishina Diwani Athumani, leo tarehe 7
Januari, 2017, na kuteketeza sehemu ya soko kuu la Kayanga wilayani
Karagwe kwa mara ya pili ikiwa limewahi kuungua,
amebainisha kuwa tayari Halmashauri ya wilaya hiyo imeshatekeleza
maelekezo yao ya kuunda timu ya uchunguzi ambayo inaanza kutekeleza
majukumu yake kesho, tarehe 8 Januari, kwa muda wa siku nne.
“Tumeunda
timu tujue kwa nini hili soko linakuwa na majanga ya moto ya mara kwa
mara, nawaomba wananchi wote wa Kayanga toweni ushirikiano wa kutosha
kwa timu hii na yeyote mwenye taarifa ya chanzo cha moto awasilishe
taarifa zake kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
hii” Alisisitiza Athumani.
Aidha,
Athumani alifafanua kuwa yeyeyote atakaye bainika kuwa ndo chanzo cha
kusababisha majanaga ya moto kutokea mara kwa mara katika soko hilo
hatua stahiki zitachukuliwa kwa kuwa kuungua kwa soko hilo kumekuwa
kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiara wa soko hilo.
Akiongea
wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,
Adeodata Agustine, amefafanua kuwa thamani ya awali ya mali
iliyoteketea inakisiwa kuwa Tsh, 80,000,000/= (mazao ya nafaka,
mbogamboga , matunda pamoja na nguo na bidhaa za dukani), na thamani ya
vibanda ni Tsh, 52,000,000/= na meza ni 9,600, 000/=.
“Chanzo
cha moto hadi sasa hakijajulikana na kikosi cha zimamoto kwa
kushirikiana na na Polisi na TANESCO wanaendelea na uchunguzi, taarifa
hii ni ya awali tutapata taarifa kamili ya thamani ya mali na chanzo
cha janga la moto baada ya timu kukamilisha kazi kwa muda uliopangwa”
alisema Adeodata.
Naye
mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko kuu la Kayanga, Wilton William,
aliishukuru halmashauri hiyo kwa juhudi walizo zifanya za kuzima moto
huo pamoja na hatua walizozichukua za kuchunguza chanzo cha moto huo
amabao umeunguza soko hilo kwa mara ya pili mfululizo.
Soko
la Kayanga lina jumla ya vibanda 257, ambapo vibanda 122 vimejengwa
kwa matofari, na vibanda 135 vimejengwa kwa mbaao. Katika tukio la
janaga la moto la mwaka jana vibanda 117 ikiwa ni viband 83 vya mbaao
na 34 vya tofari viliteketea kwa moto.
Katibu
tawala Mkoa wa Kagera Kamishina, Diwani Athumani akipata maelezo kutoka
kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Adeodata
Agustine juu ya janga la moto katika soko kuu la Kayanga alipotembelea
soko hilo kujionea athari za moto tarehe 7 Januari 2017.
Katibu tawala Mkoa wa Kagera Kamishina, Diwani Athumani (katikati) akipata maelezo ya uratibu wa majanga kutoka kwa Mkurugenzi
Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen. Mbazi Msuya
wakati alipotembelea soko hilo kujionea athari za moto tarehe 7 Januari
2017 (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe,
Adeodata Agustine.(PICHA ZOTE NA OFFISI YA WAZIRI MKUU)
Baadhi ya Wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wakipakia mabaki ya mazao yao baada ya vibanda vyao vya biashara kuungua moto kufuatia moto uliozuka usiku wa saa 9:00 usiku wa tarehe 7Januari, 2017, na kuteketeza sehemu ya soko kuu la Kayanga wilayani Karagwe kwa mara ya pili ikiwa limewahi kuungua tarehe 11 Machi 2016.
Muuonekano
wa Soko Kuu la Kayanga baada ya vibanda vya baadhi ya wafanyabiashara
kuungua moto kufuatia moto uliozuka usiku wa saa 9:00 usiku wa tarehe 7
Januari, 2017, ikiwa soko hilo limewahi kuungua tarehe 11 Machi 2016.
No comments:
Post a Comment