Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo na mgeni
wake Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kulia) Ikulu leo jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli (hayupo pichani) Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akikagua gwaride mara baada ya
kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (hayupo
pichani) Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan
akiteta jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majali (katikati) na Katibu
Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
Baadhi
ya viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Miuungano wa Tanzania (waliokaa
upande wa kulia) wakiweka saini katika mikataba na wawakilishi kutoka
Serikali ya Uturuki leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya mikataba tisa
imetiwa saini, ikiwemo ushirikiano wa kimaendeleo.
Waziri
wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Tanzania akibadilishana hati ya
makubaliano na Waziri wa Fedha wa Uturuki leo jijini Dar es Salaam.
UT5b:
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Ryoba
akibadilishana hati ya makubaliano na mwakilishi wa Serikali ya Uturuki
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akibadilishana hati ya makubaliano na Waziri wa Mambo
ya Nje wa Uturuki leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akiwapungia mkono wakazi wa jiji la Dar
es Salaam waliofika kumlaki katika viwanja vya Ikulu leo.Kushoto kwake
ni Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Baadhi
ya wananchi wakimlaki Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alipowasili
katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Rais huyo yupo nchini
kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo katika ziara hiyo Tanzania na
Uturuki wameingia makubaliano katika mikataba tisa kwa lengo la
kushirikiana na kusaidiana.
Baadhi
ya wageni walioambatana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
wakiingia katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiteta jambo
na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe walipokuta wakati
wa ugeni wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan( hayupo pichani) leo
jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa ndani ya gari na mgeni wake Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu
jijini la Dar es Salaam leo.
Rais
Dkt. John Pombe Joseph Maguli na mgeni wake Rais wa Uturuki Recep Tayyip
Erdogan (walioshikana mikono) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Mawaziri na viongozi kutoka Serikali za Tanzania na Uturuki leo jijini Dar es
Salaam.
Picha na: Frank Shija
– MAELEZO.
Na Beatrice
Lyimo-MAELEZO
Serikali ya Tanzania
na Serikali ya Uturuki zimesaini mikataba tisa ya makubaliano ya kiuchumi inayolenga
katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa maendeleo baina ya nchi hizo.
Mikataba hiyo
inahusisha sekta za uchukuzi, mawasiliano, habari, elimu, utalii, utafiti,
viwanda, afya na ulinzi.
Akizungumza mara
baada ya kusaini kwa mikataba hiyo leo
Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Magufuli alisema ujio wa Rais wa Uturuki na ujumbe wake ni kielelezo cha ukuaji
wa mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki katika nyanja ya biashara na
kimaendeleo baina nchini hizo.
Rais Magufuli alisema
katika mazungumzo yake aliyofanya na Rais Recep Erdogan kuhusu ujenzi wa Reli
ya Standard Gauge nchini, alimjulisha kiongozi huyo kuwa miongoni mwa
wakandarasi walioomba zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kuwa ni kampuni kutoka Uturuki,
hivyo endapo itashinda zabuni hiyo itasaidia kukuza uhusiano uliopo baina ya
nchi hizi mbili.
Aidha, Rais Magufuli
alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inatarajia kuomba mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki katika
kujenga sehemu ya kipande cha ujenzi wa reli hiyo.
Rais magufuli alisema
Tanzania inaendelea kunufaika na uwepo wa Shirika la Ndege la Uturuki kwa kufanya
safari zake za moja wka moja kutoka nchini Uturuki, kwa kuwa utasaidia
kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.
Kwa upande wake Rais
wa Uturuki, Recep Erdogan alisema kuwa uwepo wa mikataba hiyo baina ya Tanzania
na Uturuki itasaidia kupata matokeo mazuri ya uhusiano pamoja na fursa
mbalimbali za ushirikiano katika nyanja ya Kilimo, Utalii, Ulinzi, Reli ambazo
zitawezesha kukuza uchumi wa mataifa hayo.
Rais Erdogan alisema
kuwa Uturuki imelenga kukuza ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania kupitia makongamano ya
wafanyabiashara yenye malengo ya kukuza uchumi, kuongeza ajira pamoja na kukuza
ujasiriamali baina ya Tanzania na Uturuki.
“Kiwango cha Biashara
ya uwekezaji katika nchi ya Uturuki ni Dola za kimarekani 150 ambapo lengo letu
ni kufika Dola za kimarekani 500” alisema Rais huyo.
Aidha Rais Erdogan alisisitiza
kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia nchi hizi kusonga mbele na kufanikiwa
katika nyanja mbalimbali.
Nae Waziri wa
Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa makubaliano ya mkataba
baina ya Tanzania na Uturuki katika Sekta ya Utalii yatasaidia katika kutangaza
vivutio vilivyopo nchini, kubadilishana wataalamu, kubadilishana taarifa na kuongeza
idadi ya watalii nchini.
Prof. Magembe
aliongeza kuwa makubaliano hayo yatakuza sekta ya utalii katika kuvutia uwekezaji
wa katika maeneo ya hoteli, fukwe na mbuga za wanyama zilizopo nchini.
No comments:
Post a Comment